Je Ni Dada Wangu Au Dada Yangu

MwendaOmo

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2013
Posts
774
Reaction score
723
Kwa mda mrefu, nilikuwa nikijua kuwa tunasema "dada yangu." Lakini mda kidogo uliopita, nilikuwa nikitazama runinga ya KBC katika kipindi fulani kinachojihusisha na ukuzaji wa lugha ya Kiswahili, na huyu mhojiwa akasema kuwa mtungo sahihi ni Dada Wangu kwasababu neno "dada" liko katika ngeli ya a-wa. Je, wana JF wasemaje?
 
dada wangu?? Duh ! Btw wakenya hawajui kiswahili..
 
dada wangu?? Duh ! Btw wakenya hawajui kiswahili..

Sikuelewi mkuu; jibu ni lipi?

Je wajua Kiswahili kilizaliwa Mvita wala si Ugunja? Kile kilichotuuza ni uongozi mbaya wa kisiasa
 
Zingatia:

1.Kuku wangu...(kuku yangu X)

2.Dada yangu...(dada wangu X)
 

ukisoma vizuri ngeli kuna aina za ngeli kulingana na mitazamo tofauti,labda ye sijui anauzungumzia upi?ila nnachofaham mm ni dada yangu ni kiswaili sanifu,kwani unapotaka kutumia upatanisho wa kisarufi utasema dada yangu analima{umoja} pia utasema dada zangu wanalima{uwingi}utapata ngeli ya a_wa pia ukimchukua paka utasema paka wangu analia{umoja}pia utasema paka wangu wanalia{uwingi} utapata pia ngeli ya a_wa sasa kumbe ktk ngeli itategemea nani unaemzungumzia kati ya mtu au kitu,lakini pia tukumbuke kuna udhaifu katika kila ngeli huo pia ni udhaifu wa ngeli ya upatanisho wa kisarufi,huo ndo mtazamo wangu labda tujifunze kwa wadau wengine.
 
Sikuelewi mkuu; jibu ni lipi?

Je wajua Kiswahili kilizaliwa Mvita wala si Ugunja? Kile kilichotuuza ni uongozi mbaya wa kisiasa

hapana,ungesema kingozi kidogo ningekuelewa,lakini tatizo sio kuzalia tatizo ni jamii ngapi zinafanana ktka matamshi na matumizi kiunguja kilikuwa na sifa ya kueleweka kwa ukaribu na jamii nyingi ndomana kikasanifiwa.
 

Aliyekuwa akinena haya alikuwa mwalimu wa shule fulani ya msingi, na nikidhani ni mwanafunzi wa yule mwandishi wa Kitanzania Wallah Bin Wallah. Kwa kweli aliponena hayo nilishangazwa sana. Lakini nilipokuja kuitazama kwa undani, niliona ukweli kiasi fulani. Kwa mfano, twasema, "mtoto wangu," ingawa mtoto si mnyama bali ni mtu. "Mke wangu" na "Mme wangu" Kwanini basi baba, mama, bibi ziwe tofauti? Na bwana je? Twasema "Bwana wangu" Kwanini tuje tusememe bibi yangu? Mjomba, Mchumba - wote ni wangu.
 
Kwa akina sie hapa ndio tunachanganyikiwa kabisa. Kiswahili kigumu.
 
Hapa ndio nazidi kuchanganyikiwa zaidi,,,,,,,,dada wangu...!!!
 

changamoto!ngoja turudi darasani
 
mi nnachokiona hapo upatanisho wa kisarufi unakuwepo lakini kuna excemption katka baadhi ya maneno mfano baba, mama,bibi,shangazi n.k zipo katika ngeli ya YU-A-WA ingawaje hazikidhi tofauti na mtoto,mjomba,kijana n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…