JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
JE, DATA GANI ZINAPASWA KULINDWA CHINI YA SHERIA YA ULINZI WA DATA?
Sheria ya #UlinziWaData ambayo bado haipo nchini Tanzania inaumuhimu mkubwa kwasababu itasaidia kulinda #Data kama zifuatazo:
Majina ya Watu(Wateja kama ni kwenye Kampuni ya biashara), Anuani za Posta na Makazi za Wananchi ambao na Wateja wa Makampuni ya biashara
Barua pepe za watu, hii inajumuisha mawasiliano yote yanayaofanyika kwa njia ya barua pepe na kufanikishwa chini ya uwezeshaji wa mtoa huduma
Namba za simu pamoja na mawasiliano yote yanayofanyika kupitia njia ya simu chini ya Kampuni zinazotoa huduma ya mawasiliano ya simu
Taarifa za Kibenki na miamala yote inayofanyika kupitia Taasisi za Fedha. Sheria itazitaka Kampuni husika kuhakikisha taarifa za wateja wao zinatunzwa
Taarifa za afya za Watu, taarifa hizi hukusanywa na Taasisi mbalimbali zinazotoa huduma ya afya pamoja na mashirika yanayotoa Bima za Afya
Data zozote ambazo ambazo watoa huduma hasa za Kibiashara wanakusanya na kuhifadhi kidijiti zinahitaji kulindwa vizuri. Katika mataifa yaliyotangua kuandaa sheria ya Ulinzi wa Data tayari wao wana muongozo wa njia bora ya kutunza na kutumia data wanazokusanya.
SHERIA
Sheria ya Ulinzi wa Data inaweka vigezo na muongozo wa namna bora Asasi za Kiraia, Serikali na Makampuni ya Biashara yanapaswa kuzingatia namna bora ya kutunza na kulinda taarifa/data za watu au wateja wao. Utunzaji unahusisha kuhakikihsa Data hizo ni Sahihi, Salama, na hazijavunjwa sheria.
Kanuni za utunzaji wa Data zinaeleza yafuatayo:
- Data zinatumika kama ilivyoelekezwa
- Data hazitunzwi kupita muda uliowekwa kisheria na bila ya ulazima
- Zinatumika kwa usahihi
- Zimetunzwa vizuri na kwa usalama
- Zinatumika kwa kufuata sheria
- Hazitumwi nje ya eneo la kiutawala bila ya kufuata kanuni nataratibu
Upvote
0