mzulumanga
New Member
- Jun 1, 2011
- 1
- 5
Itakuwa ni jambo la kustaajabisha endapo hata kwa bahati mbaya haujawahi kukutana na moja ya msemo miongoni mwa misemo ifuatayo: “elimu ni ufunguo wa maisha”, “elimu ni mwanga”, “elimu ni ukombozi”. Ninapata nguvu ya kueleza hicho nilichoeleza kwa maana misemo hiyo michache na mingine mingi inayofanana na hiyo; ni miongoni mwa misemo maarufu sana hapa nyumbani kwetu Tanzania kwasababu imekuwa ikitumika kama kauli mbiu “motto” kwenye shule mbali mbali hapa nchi Tanzania.
Kwa kuwa lengo kuu la elimu ni kuhakikisha kwamba mwanadamu anapata maendeleo endelevu katika maisha yake, hivyo nina matumaini makubwa kwamba waanzilishi na watunzi wa misemo hiyo walikuwa na dhamira njema, tena njema sana; dhamira ya kuchochea ari, kuhimiza, kuamsha shauku na kuhamasisha watoto wao, vijana wao na watu wote kiujumla kuitafuta na kuishika elimu kwa bidii na kwa hali na mali.
Hata hivyo, hapa kuna maswali kadha wa kadha ya kujiuliza; “Je, elimu imekuwa ufunguo wa maisha kweli?” “Je, elimu imekuwa ni mwanga kweli?” “Je, elimu imekuwa ukombozi kweli?” La hasha! “Je, changamoto ni nini?”
Awali ya yote tuangazie tafsiri ya neno “elimu” kama lilivyotafsiriwa na kamusi ya lugha ya Kiswahili pamoja na baadhi kwa wanazuoni japo kwa uchache ili sote tusafiri kwenywe mtumbwi mmoja.
Kamusi ya Longhorn inalitafsiri neno “elimu” kama, “maarifa yanayotolewa kwa mfumo maalum wa kufundishia na kujifunzia.”
Aidha, kwa mujibu wa Knowels “Elimu ni ukuzaji wa uwezo wote uliomo ndani ya mtu binafsi utakaomwezesha kudhibiti mazingira yake na kutimiza wajibu wake.”
Licha ya tafsiri hiyo ilitoyolewa na Knowels mwaka 1995, Aristotle alitafsiri maana ya neno “elimu” kabla ya ujio wa Kristo kama, “mchakato wa kumfundisha mwanadamu kutimiza azma yake kwa kutumia uwezo wote kwa ukamilifu kama mwanajamii.”
Hivyo, kwapamoja tunaweza kukubaliana kwamba elimu ni mchakato wa kuwezesha kujifunza, au kuwezesha upatikanaji wa maarifa, ujuzi, maadili, imani, na tabia. Au tunaweza kusema elimu ni kuboresha uwezo huo wote kwa mtu binafsi ambao humwezesha kudhibiti mazingira yake na kutimiza wajibu wake.
Kulingana na tafsiri hizo za neno “elimu” nilizoeleza hapo juu, ni wazi kwamba elimu inaweza kupatikana kwa mtindo ulio rasmi “formal education” na kwa mtindo usio rasmi “informal education”. Lakini yote kwa yote duniani kote ikiwemo Tanzania inakubalika kwamba elimu ndiyo silaha kubwa na muhimu katika harakati za kupunguza umaskini na kuinua maisha bila ya kujali imepatikatana kwa mtindo upi. Na hilo linathibitishwa kwenye kitabu kitakatifu cha Biblia, “mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.”(Mit 4:13)
Hata hivyo, licha ya kulitambua hilo lakini bado tumeendelea kuwa na wasomi ambao wanaendelea kuteseka katika dimbwi la umaskini na ufukara mkubwa kwa maana hawana ajira na wameshindwa kutumia elimu zao kupata vipato.
Lakini pia wapo wale ambao elimu zao hazijawasaida lolote kwa maana hawajastaarabika kulingana na viwango vya elimu zao. Na ndio maana sio jambo la kushangaza kumkuta msomi wa chuo kikuu akijisaidia sehemu isiyo rasmi au akishiriki kung’oa viti kwenye uwanja wetu wa taifa.
Ukiachana na hao, wapo wale ambao wamemaliza elimu zao, wana vyeti ila vichwani mwao ni kweupe na hawana tofauti na jinsi walivyokuwa kabla ya kuanza kupatiwa elimu. Kwani ni mara ngapi tumekuwa tukisikia taarifa za watoto wanaomaliza darasa la saba wakiwa hawajui kusoma wala kuandika??
Nikiyatafakari hayo huwa najikuta nikibun’gaa bung’aa na kujiuliza mwenyewe, “Je, kinachotolewa hapa nchini kwetu tanzania ni elimu bora au bora elimu?” Kisha hujijibu mwenyewe, “ bila shaka kinachotolewa hapa nchini kwetu ni bora elimu!”
Nimesema ni “bora elimu” kwasababu, elimu ambayo inatolewa hapa kwetu Tanzania ni ile inayomtayarisha mtoto kwa ajili ya kujipima na mitihani tu na si kwaajili ya maisha. Wakati “elimu bora” ni ile inayomlenga mtoto kwa ujumla, yaani makuzi ya kijamii, kihisia, kimwili na kiakili ya kila mwanafunzi bila kujali jinsia, rangi, kabila, hali ya kijamii na kiuchumi, au eneo la kijiografia. Elimu bora, inamtayarisha mtoto kwa maisha, si kwa ajili ya kujipima na mitihani tu.
Licha ya hayo yote, bado tunayo nafasi ya kuziba ufa kabla hatujajenga ukuta. Tunachopaswa kufanya ni kubaini tatizo lilipoanzia na kisha kulitatua.
Natamani ningekuwekea hapa historia fupi ya elimu nchini Tanzania kabla ya uhuru na baada ya uhuru. Ila kwa leo ninapenda kukueleza kwa kifupi tu kwamba, tangu tupate uhuru tumepiga hatua kubwa sana kwa kuwa tumefanikiwa kubadili mfumo wa elimu kutoka kwenye mfumo wa elimu uliokuwa na lengo la kupata watumishi Waafrika ambao wangetumika katika kutetea matakwa ya wakoloni, na hivyo kuwafanya wasomi kuwa tegemezi, mpaka kufika kwenye mfumo wenye manufaa kwa Watanzania wote bila ubaguzi.
Pamoja na mafanikio hayo yote, ipo wazi kwamba mfumo wetu wa elimu bado unasua sua sana kutokana na changamoto lukuki. Hivyo, kwakuwa mimi ni mdau muhimu wa maendeleo ya taifa langu la Tanzania na mwenye haki ya msingi ya kutoa maoni (kwa mjibu wa ibara ya 18(1) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa mabadiliko mara kwa mara, ibara hiyo ninainukuu hapa chini kama ifuatavyo; “ bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.”), nitayaainisha na kuyaelezea hapo chini maeneo muhimu ambayo yakiboreshwa zaidi yatasaidia watoto wa mama Tanzania kupata “elimu bora” kwa kiasi fulani kwakuwa upatikanaji wa elimu bora unategemea mambo mengi sana na hivyo tunapaswa kukabiliana na changamoto zote hatua kwa hatua.
Mosi; lugha ya kufundishia imekuwa changamoto kubwa sana kwa waalimu, wanafunzi na wazazi pia. Jambo ambalo linapelekea utoaji na upatikanaji wa elimu isiyo bora nchini Tanzania. Hivyo Serikali inawajibu wa kutafuta suluhu ya kudumu ili kuhakikisha kuwa lugha ya kufundishia inafahamika vyema kwa walimu na wanafunzi. Ama lugha ya Kiswahili iwe lugha rasmi ya kufundishia na kujifunzia kuanzia elimu ya awali, sekondari na hata elimu ya juu au Lugha ya Kingereza iwe lugha rasmi ya kufundishia na kujifunzia kuanzia elimu ya awali, sekondari na hata elimu ya juu. Endapo lugha ya Kingereza itaonekana kufaa zaidi; basi nitashauri kwamba, “kwakuwa lugha ya Kingereza hapa nchini kwetu ni lugha ya pili au ya tatu, hivyo serikali itapaswa kuboresha mbinu za ufundishaji wa somo la Kingereza kwamaana hivi sasa somo hilo linafundishwa kitaaluma zaidi na halijajikita sana kwenye mawasiliano jambo linalopelekea wanafunzi wengi kushindwa kumudu lugha hiyo.
Alkadhalika, kumekuwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa madarasa, maabara, madawati, vitabu, nyenzo na vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Kwasababu hiyo, Serikali inajukumu la kuhakikisha kuwa shule zote zina madarasa, maabara, madawati, vitabu, nyenzo na vifaa vya kufundishia na kujifunzia vya kutosha wanafunzi wote ili wanafunzi waweze kujifunza vizuri bila vikwazo vya aina yeyote. Na isiwe bora madarasa ama bora maabara ama bora madawati ILA yawe madarasa, maabara na madawati yenye viwango bora. Vilevile ikumbukwe kuwa vitabu ndiyo kiongozi mkuu kwa walimu na wanafunzi; hivyo Serikali inapaswa kuifanyia marekebisho sera ya matumizi ya vitabu vya kiada iliyopo kwa sasa ili iwe kama ilivyokuwa zamani ambapo kitabu cha aina moja chenye ubora kilikuwa kinatumika nchi nzima. Endapo kutakuwa na ulazima wa ktumia vitabu vya ziada, basi Serikali ipendekeze vitabu vitakavyofaa kutumika kwa maana kuna baadhi ya vitabu ambavyo havina ubora unaohitajika, jambo linalofanya wanafunzi wajifunze dhana zinazotofautiana.
Sambamba na hilo, Serikali inapaswa kuhakikisha inaunda mfumo bora wa mafunzo utakao waandaa waalimu ambao watakuwa na sifa nzuri za kitaaluma na moyo wa kujitolea. Lakini pia, wakaguzi wanapaswa kufika shuleni mara kwa mara ili wathibitishe kama elimu inayotolewa ni bora na inaendana na mtaala au elimu inayotolewa ni ya hovyo, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa mapema iwezekanavyo. Tena, Serikali inapaswa pia kuboresha maslahi ya waalimu ikiwemo kuwapandisha madaraja, kuongeza mishahara, kuwapatia nyumba za kuishi, mazingira mazuri ya kazi, kutoa zawadi kwa wale walionyesha jitihada binafsi, na kuwapatia semina na kozi fupifupi ili kuwapa motisha, kuwatia moyo na kuwaboresha zaidi.
Mbali na hayo, Serikali inapaswa pia kuboresha Mitaala yetu. Amini usiamin, ni ngumu sana kukwepa kusikia simulizi za ukosefu wa ajira huko mitaani kwa kuwa kilio ni kikubwa mno. Ili tuondokane na sakata hilo, ni vema kama Serikali ikaboresha mitaala yetu kwa kuongeza masomo yatakayotoa ujuzi na maarifa mbalimbali kama vile ufundi, kilimo na biashara ili kuwawezesha wahitimu kujitegemea, kujiajiri na kumudu changamoto kwenye jamii zao pindi watakapohitimu elimu zao.
Yote kwa yote, naamini mtakubaliana na mimi kwamba hizo changamoto nilizozieleza hapo juu sio ngeni masikioni mwenu. Hivyo, nitatoa rai yangu kama ifuatavyo:
Serikali; Sasa umefika wakati wa kutatua changamoto hizo bila kupepesa macho kwa maana mambo hayo yameshaongelewa sana na kwa muda mrefu bila hatua stahiki kuchukuliwa. Pamoja na hilo, serikali lazima itambue kuwa inawajibu wa kuhakikisha kwamba ili shule ifunguliwe na iendeshwe kama shule ni lazima ikidhi viwango vinavyokubalika. Vilevile, itoe mgawanyo sawa wa rasilimali za taifa kwenye elimu unaozingatia haki za watoto wote wa Tanzania.
Wanasiasa; Ni lazima mtoe maamuzi yatakayo lenga katika kuboresha utoaji wa elimu bora na siyo kuibua ubishi na mashindano yasiyo na tija katika maendeleo ya sekta ya elimu nchi.
Wazazi; mnawajibu wa kuhakikisha kuwa watoto wao wanaenda shuleni na mnafuatilia maendeleo yao mara kwa mara kwa kila hatua.
Jamii; lazima itambue kuwa mototo wa mwenzako ni wako, hivyo isijitenge katika malezi ya watoto wa mama Tanzania hususani katika kuhakikisha wanapata elimu bora.
Waalim; mnajukumu la kufanya kazi yenu kwa moyo wote, maadili na nidhamu mkijua ya kwamba mchango wenu ni mkubwa sana katika taifa. Mkiandaa wataalam wa hovyo, hivyo tutakuwa na taifa la hovyo na duni.
Wanafunzi; mnapaswa kufuata maelekezo mnayopewa na wazazi na waalimu wenu, ikiwa ni pamoja na kuwa na nidhamu, kuhudhuria masomo, kusoma kwa juhudi na kuhakikisha mnafaulu.

Upvote
1