Leo katika kuangalia angalia habari za nyumbani nilikongoli tofuti ya Darhotwire.com na picha niliyokutana nayo ni basi la Daladala huku wanafunzi kibao wakijitahidi kuingia ndani ya basi hilo bila mafanikio.
Nikaanza kujiuliza maswali mengi sana kichwani mwangu ambayo majibu yake mengi tunayo. Ila kwa mtanzania wa kawaida aliyekaa nyumbani (Tanzania) muda wote bila kusafiri safiri anaweza kuwatupia kwa asilimia 90 wamiliki wa Daladala,..., hata mwandishi wa habari ile naye vile vile alikuwa anawatupia wamiliki hao kwa tatizo hilo..,
Je wadau hilo ni sawa? Ninaweza kuwa nimepotoka ila mimi msimamo wangu ni mwingine kabisa.
Kwanza ikumbukwe huko nyuma ni mkoa wa Dar es salaam tu ndio uliokuwa na utaratibu wa magari ya usafiri ndani ya Jiji maarufu kwa jina la UDA, ila wateja walivyazidi kuwa wengi serikali ilitoa uhuru kwa watu binafsi KUSAIDIA hapo ndio yakaanza madaladala na nauli ilikuwa ni shilingi tano (au Dala) chanzo cha magari hayo kuitwa hivyo.
Ila kadri siku zinavyozidi kujongea serikali ilianza kujitoa taratibu na matokeo yake DalaDala ndio zinakwa tegemezi na UDA zinasaidia pale Daladala zinaposhindwa kukidhi haja.., Kwa mtazamo wangu hili sio sahihi kabisa.
Pamoja na kwamba serikali imeamua kujitoa katika biashara na jukumu lake limebaki katika kukusanya Kodi tu, ila Huduma muhimu kama usafiri si vizuri likategemea kwa asilimia 95 usafiri binafsi.
Katika nchi nyingi Duniani suala la usafiri ndani ya miji ni la serikali na watu binafsi wanakuwa na magari yao ambapo wananchi hupanda kwa gharama ya juu kidogo ukilinganishwa na yale ya serikali. katika magari haya binafsi yanakuwa na ubora wa juu zaidi humu hakuna cha mwanafunzi wala mzee wote hulipa nauli sawa, ila yale ya serkali kunakuwa na bonus mbali mbali kuanzia wanafunzi, na katika nchi nyingine kama Urusi, Korea, Sweden hata senior citizen (Wastahafu na wazee) wanakuwa na punguzo lao vile vile, kwani ni jukumu la serikali moja kwa moja kutoa huduma kwa mafungu hayo mawili niliyoyataja.
Nakutolea mfano mmoja hapo hapo Tanzania mbona wazee na watoto chini ya miaka mitano katika Hospitali za serikali wanakuwa na punguzo?, ukienda hospitali binafsi hilo lipo? (haiwezekani kwani asilimia 60 ya wagonjwa wanaangukia fungu hilo hivyo Hospitali zingekuwa zinaendeshwa kwa hasara).., sasa kwanini Leo tumlazimishe mwenye Daladala anayelipa kodi serikalini kwa biashara hiyo kubeba mzigo wa serikali?..,
Cha maana hapa ili kuondoa hili tatizo ni Serikali kujikita katika kuboresha huduma hii na kuongeza magari yake binafsi... , Hivi Daladala wakigoma hata kwa wiki moja Serikali itahakikisha vipi wafanyakazi wake wanafika kazini kwa wakati nila kuathiri utendaji kazi mzima wa Serikali.
Kama tunataka watoto wetu wasome katika mazingira mazuri na kuondokana na tatizo hili serikali iache kabisa kutegemea watu binafsi katika suala hili...
Mimi kwa leo nawasilisha sijui wana jamii mnasemaje?