Matojo Cosatta
JF-Expert Member
- Jul 28, 2017
- 234
- 390
JE NI HALALI KISHERIA KWA BABA KUKATAA KUMRITHISHA MALI MTOTO WAKE WA KUMZAA?
SEHEMU I: UTANGULIZI
Kuna imani kubwa imejengeka miongoni wa raia wa kawaida wa Tanzania na hata kwa baadhi ya wanasheria kuwa mtu ana haki ya moja kwa moja (automatic right) ya kurithi mali ya mzazi wake baada ya kifo cha mzazi (Baba au Mama) na mzazi ana wajibu wa lazima kisheria kuwarithisha mali watoto wake na mke wake. Huu mtizamo ni sahihi kabisa kisheria kwa urithi unao ongozwa na Sheria za Kimila na Sheria za Kiislam na urithi unao ongozwa na Sheria zilizotungwa au kuidhinishwa na bunge (statutory laws) ambapo marehemu amekufa bila kuandika wosia lakini mtizamo huu sio sahihi kwa urithi unao ongozwa na statutory laws iwapo marehemu ameacha wosia.
Je kisheria mtu anayo haki ya moja kwa moja ya kurithi mali za mzazi wake baada ya kifo chake?
Au kwa maneno mengine, je mzazi anaweza kumnyima urithi mtoto?
Kwa madhumuni ya kujua jibu sahii la swali hili ni muhimu kujua kuwa maswala ya urithi (succession) nchini Tanzania linana ongozwa na sheria za aina 3 nazo ni;
(1) Sheria zilizotungwa au kuidhinishwa na bunge (statutory laws)
(2) Sheria za Kiislam
(3) Sheria za Kimila
Ni muhimu kujua mambo matatu (3) yafuatayo. Kwanza, sheria za Kiislam zinatumika katika urithi na mgawanyo wa mali za marehemu kwa Waislam. Pili, sheria za mila zinatumika kwa watu wanaoishi mfumo wa maisha wa mila, desturi na tamaduni za kabila fulani ambao wengi wao wanaishi vijijini. Tatu, sheria zilizotungwa au kuidhinishwa na bunge (statutory laws) zinatumika katika urithi na mgawanyo wa mali za Wakristo na watu ambao hawana imani za dini (wapagani) au watu wanaoishi mfumo wa maisha ya kisasa ambao hafungamani na dini yoyote au kabila lolote (Wakisasa).
Swala la mtu kuwa na haki ya kurithi mali linategemea na sheria itakayotumika katika urithi na mgawanyo wa mali za marehemu na nilinategemea iwapo marehemu aliandika wosia au hakuandika wosia. Iwapo Sheria za bunge (statutory laws) zitatumika katika urithi na mgawanyo wa mali za marehemu basi Mzazi kupitia Wosia ana uwezo kisheria wa kumnyima urithi mtoto wake wa kumzaa au mke wake wa ndoa lakini chini ya sheria za Kiislam na Sheria za mila mzazi hana kabisa mamlaka ya kumnyima urithi mke wake ndoa au mtoto wake kumzaa na kumpatia urithi mtu baki yoyote anayemtaka. Hatahivyo, katika sheria za urithi za mila kuna mazingira fulani ambapo sheria inampa uwezo mzazi kumnyima urithi mtoto wake iwapo mzazi atatoa sababu za kumnyima mtoto urithi zinazokubalika kisheria ikiwemo mtoto kumpiga mzazi, kutembea na mke wake na kutomtunza au kumtelekeza wakati wa ugonjwa au uzee.
Pia, ni muhimu kuzingatia kuwa kila mtu ana haki ya moja kwa moja ya kurithi mali za mzazi wake iwapo mzazi amekufa bila kuandika wosia (intestacy) bila kujari sheria ipi inatumika katika kurithisha mali za marehemu lakini iwapo mzazi ataacha wosia (testacy) basi anaweza kumnyima urithi mtoto wake katika sheria za mila na sheria za bunge. Chini ya sheria ya statutory law mzazi mkristo, mpagani au mkisasa akimnyima mtoto au mke urithi kwa wosia hawajibiki kutoa sababu.
SEHEMU II: SHERIA ZA KIISLAM
Sheria za Kiislam kwenye maswala ya urithi zimejenjwa katika jurisprudensia (falsafa ya sheria) ya "Doctrine of Forced Heirship" yaani Kunga ya Urithi wa Lazima. Dhana au Kunga (principle) hii ya Forced Heirship ina mlazimisha mzazi kurithisha mali zake kwa mke wake, watoto wake na ndugu zake wa damu na iwapo mzazi kwa njia ya wosia atarithisha mali zake kwa watu baki ambao sio ndugu wa damu basi Wosia wake au urithisho wake utakuwa batili kisheria (void) na mali zitagawiwa upya kwa mke, watoto na ndugu wa marehemu kwa kufuata kanuni za mgawanyo wa mali za marehemu kwa mujibu wa sheria za Kiislam za urithi kana kwamba marehemu hakuandika Wosia wowote.
Kwa sheria ya Kiislam, nitakwa la Haya ya 11 na 12 ya Surat Nisa ya Kuruani Tukufu kuwa Mwiislam lazima arithishe mali zake kwa mke, wototo, na ndugu zake wa damu akiwemo baba, mama, kaka na dada n.k. Mtoto wa kiume anapashwa kupata mara 2 ya mtoto wa kike na kama warithi ni watoto wa kike pekee basi watarithi mbili ya tatu (2/3) ya mali ya marehemu na kama wa kike ni mmoja basi atapata nusu (1/2) na Mke anapata moja ya nane (1/8) na mwanaume anapata robo (1/4) ya mali ya mke wake. Swala la mgawanyo wa mali za marehemu kwa kutumia sheria za Kiislam ni pana sana na linaitaji makala inayojitegemea, hivyo, sitaenda kwenye undani wa swala hili.
Hatahivyo, Mwislam anaruhusiwa kurithisha mali kwa watu ambao sio ndugu wa damu (watu baki) kwa njia ya wosia kwa masharti kwamba urithi ambao watu baki watapata husizidi moja ya tatu (1/3) ya mali za marehemu mzazi na ndugu wa damu na mke wa marehemu lazima wapate urithi usiopungua mbili ya tatu (2/3), na hili sharti ni kwa mujibu wa Hadith ya Mtume Muhammad (S.A.W.) ambayo ilihadithiwa na Sa'd bin Abi Waqqas ambayo ni Hadith No. 725 katika kitabu cha Sahihi Bukhari, Vol. 8, Book No. 80, hiki ni chanzo cha kuaminika sana cha Hadith za Mtume Muhammad katika Dini ya Kiislam ni mojawapo ya Kutub al-Sittah kuhusu maneno na matendo ya Mtume wa Mungu. Iwapo Muislam atarithisha mali zake kwa watu baki zaidi ya 1/3 basi mali yote inayozidi 1/3 ni batili na itarudishwa kwa ndugu wa damu wa marehemu.
SEHEMU III: SHERIA ZA MILA
Pia, sheria za mila kwenye maswala ya urithi zimejengwa katika jurisprudensia (falsafa ya sheria) ya "Doctrine of Forced Heirship" (Kunga ya Urithi wa Lazima) kama zilivyo sheria za Kiislam kwenye eneo hili. Hivyo basi, mzazi anayerithisha mali zake kwa mujibu wa sheria za mila analazimishwa na sheria za mila kurithisha mali kwa mke wake, watoto wake au ndugu zake wa damu. Msingi wa kisheria wa wa dhana hii katika sheria za mila ni sheria mahususi za kabila la marehemu husika na sheria ya nchi inayoitwa the Local Customary Law (Declaration) (No. 4) Order, 1963 (G.N. No. 436 of 1963) hususani Jedwali la Pili la sheria hii.
SEHEMU IV: SHERIA ZA BUNGE.
(i) Utangulizi
Kirai "Sheria za bunge" katika makala hii kimetumika kumaanisha sheria zilizotungwa na bunge moja kwa moja au zilizotungwa na mamlaka iliyokasimishwa na bunge pamoja na sheria za nchi za nje (received laws) zilizopokelewa kupitia sheria iliyotungwa na bunge na sheraia za bunge kwa Kiingereza zinaitwa statutory law.
Sheria ya bunge inayotumika katika urithi na mgawanyo wa mali za Wakristo na watu ambao hawana imani za dini ( wapagani ) au watu wanaoishi mfumo wa maisha ya kisasa ambao hafungamani na dini yoyote au kabila lolote ( wakisasa ) ni sheria inaitwa the Indian Succession Act, 1865, hii sheria ni ya India ya mwaka 1865 ambayo iridhinishwa na bunge kutumika Tanzania kupitia Kifungu cha 14 cha sheria inayoitwa the Judicature and Application of Laws Act, Cap. 358 pamoja na Jwedwali la Pili la sheria hii.
(ii) Msingi wa Kifalsafa wa Kunga ya Uhuru wa Kurithisha.
Sheria ya the Indian Succession Act, 1865 imejengwa katika jurisprudensia ya “Kunga ya Uhuru wa Kurithisha” mali ambapo kwa Kiingereza inatwa “Doctrine of Testamentary Freedom".
Msingi mkuu wa dhana hii ya "Testamentary Freedom" ni Haki ya Kumiliki Mali Binafsi (Right to Own Private Property) ambayo inampatia mtu au mmili haki na uhuru wa kutumia mali yake kadri atakavyo ikiwemo haki ya kumgawia au kumrithisha mali hiyo kwa mtu mwingine amtakaye kwa uhuru bila kuwekewa masharti na mtu mwingine na bila kushurutisha na mtu yoyote au mamlaka ya nchi. Dhana ya "Testamentary Freedom" ni zao la dhana ya falsafa ya uchumi wa kibepari wa magharibi na kunga zake ambazo zilipewa majina kama kadhaa kama vile liberty of estate, laissez-faire na economic freedom. Kwa ujumla ninaweza kusema kuwa dhana ya "Testamentary Freedom" ni matokeo ya kuanguka kwa mfumo kikabaila (feudalism) na ujio wa mfumo wa kibepari wa magharibi sanjari na falsafa na kunga za kiuchumi za ubepari wa kimagharibi huko bara la Ulaya hususani Uingereza. Hii dhana ya "Testamentary Freedom" pamoja na mambo mengine ni zao la ushawishi wa wanafalsafa maarufu huko Ulaya akiwemo John Stuart Mill, John Locke, Jeremy Bentham, David Recardo, Adam Smith, William Blackstone na Hugo Grotius .
Mwanafalsafa John Stuart Mill kitabu chake cha mwaka 1848 katika kiitwacho "Principles of Political Economy" anasema kuwa;
Pia, Mwanafalsafa John Locke katika kitabu chake "Two Treatise of Government" cha mwaka 1690 anasema kuwa;
Mwanafalsafa Hugo Grotius ameeleza dhana hii katika kitabu chake cha mwaka 1631 kiitwacho "The Jurisprudence of Holland". Dhana hii ya "Testamentary Freedom" inampa mzazi haki na huru wa kurithisha mali yake yote kwa mtu yoyote amtakaye hata kama ni mtu baki ambaye sio ndugu yake wa damu.
(iii) Msingi wa Kisheria wa Kunga ya Uhuru wa Kurithisha.
Katika Tanzania, msingi wa kisheria wa dhana ya Uhuru wa Kurithisha ni common law yaani hukumu za mahakama za Uingereza pamoja na Kifungu cha 46 cha the Indian Succession Act, 1865. Kifungu cha 46 kimpatia kila mtu akiwemo mzazi haki na uhuru wa kurithisha mali zake kupitia wosia kwa masharti kwamba mtu au mzazi huyo awe na akili timamu na awe na umri wa miaka 18 au zaidi. Tofauti na Sheria za Kiislam na Sheria za Mila, Sheria ya the Indian Succession Act, 1865 haijaweka sharti lolote kumlazimisha au kumshurutisha mzazi kurithisha mali zake kwa mke wake, watoto na ndugu wa damu bali sheria imempatia huru na haki ya kurithi mali zake na sheria hiko kimya kwenye swala la haki ya lazima ya mke na watoto wa marehemu kurithi za mali za marehemu mme au mzazi/baba.
Pale ambapo sheria ya Tanzania iko kimya au kuna pengo (lacuna) kuhusu swala lolote la kisheria basi tunaelekezwa kutumia Sheria za Uingereza (statutes of general application in England) au common law na Doctrine of Equity yaani Maamuzi wa Mahakama za Uingereza (Superior Courts) kama yalivyokuwa au kama sheria zilivyokuwa tarehe 22 July, 1920 na kurudi nyuma bila kikomo, hii ni kwa mujibu wa Kifungu cha 2 (3) cha sheria inayoitwa the Judicature and Application of Laws Act, Cap. 358 kama kilivyotafsiri na Mahakama ya Rufaa katika Kesi ya Issa Athman Tojo Vs Republic [2003] TLR 119. Kutokana na ukimya wa sheria ya the Indian Succession Act, 1865 kuhusu swala la haki ya lazima na ya moja kwa moja ya mke na watoto kurithi mali za marehemu mme au mzazi, basi ninalazimika kwenda Uingereza kutafuta sheria na uamuzi wa Mahakama za Uingereza kuhusu swala hili.
Kifungu cha 3 cha Sheria ya Wosia ya Uingereza ya 1837 (the Will Act, 1837) kinampa kila mtu akiwemo mzazi haki ya kurithisha mali zake kwa mtu yoyote amtakaye na chini ya kifungu hiki mzazi anaweza kumnyima urithi mtoto wake wa kumzaa au mke wake wa ndoa na kifungu hiki kinatumika Tanzania kwa sababu sheria ya Tanzania hiko kimya kwenye swala hili.
Kwa upande wa Common Law ya Uingereza, Jaji Mkuu wa Uingereza wa wakati huo, Mtukufu Cockburn mwaka 1870 katika kesi ya Banks v Goodfellow (1870) 5 LR QB 549 kuanzia ukrasa wa 563 mpaka 565 aliamua kuwa mzazi ana mamlaka yasiyokuwa na mipaka ya kurithisha mali zake kwa wosia na katika kesi hii Mahakama iliamua kuwa Wosia wa John Banks ni halali kisheria pamoja na kwamba ulimnyima urithi mtoto wake na badala yake kumrithisha mali yake yote kwa mpwa wake Margeret Goodfellow. Msingi mkuu au jurisprudensia ya kesi ya Banks v Goodfellow (1870) 5 LR QB 549 ilikuwa ni Kunga ya Uhuru wa Kurithisha Mali au Doctrine of Testamentary Freedom. Jaji Mkuu, Cockburn katika kesi ya Banks v Goodfellow (1870) 5 LR H.L. 549 katika ukrusa wa 563 alisema maneno yafuatayo:
Hii kesi ya Banks v Goodfellow (1870) 5 LR H.L. 549 imefanyiwa rejea sana na mahakama za Uingereza kuliko kesi zote katika eneo hili la Uhuru wa Kurithisha mali ikiwemo kesi ya Masterman-Lister Vs Brutton & Co & Another [2003] 3 All ER 162 na Key Vs Key & Another [2010] 1 WLR 2020 nakadhalika. Mahakama ya Juu (Supreme Court) ya Uingereza mwaka 2017 katika kesi maarufu sana ya Llott Vs the Blue Cross & Others [2017] UKSC 17 iliamua kuwa dhana ya Testamentary Freedom ni sehemu ya sheria za Uingereza na mmiliki wa mali ana huru wa kurithisha mali zake kwa mtu amtakaye kupitia wosia. Banks v Goodfellow (1870) 5 LR QB 549 ni kesi maarufu sana huko Uingereza na ni moja wapo ya msingi mkuu wa kisheria wa dhana ya Testamentary Freedom na inatumika Tanzania kwa sababu ni kesi ambayo ilifanyiwa uamuzi mwaka 1870 ambayo ni kabla ya 22 July, 1920.
Hatahivyo, iwapo Mkristo, wapagani au mkisasa atakufa bila kuandika wosia basi ni takwa la kisheria kuwa mali zake zote lazima zirithiwe na mke na watoto wake ambapo mke atapata 1/3 na watoto watagawana kwa usawa (equally) 2/3 inayobaki na kama mtoto ni mmoja basi atachukua 2/3 yote na kama marehemu hana watoto basi mke atachukua 50% na ndugu watagawana 50% iliyobaki, hii ni kwa mujibu wa Kifungu 26 na 27 cha the Indian Succession Act, 1865. Swala la mgawanyo wa mali za marehemu kwa kutumia sheria ya the Indian Succession Act, 1865 iwapo marehemu hakuandika wosia ni pana na linaitaji makala inayojitegemea, hivyo, sitaenda kwenye undani wa swala hili.
Makala hii imeandikwa na Matojo M. Cosatta na kwa mwenye maoni, maswali au anaitaji ufafanuzi kuhusu swala lolote kwenye makala hii mwandishi anapatikana kwa barua pepe ifuatayo: cosatta9@gmail.com

"haki ya kumiliki mali haiwezi kukamilika bila ya mmiliki wa mali kuwa na uwezo kurithisha mali zake kwa uhuru kadri atakavyotaka wakati wa kifo chake".
Pia, Mwanafalsafa John Locke katika kitabu chake "Two Treatise of Government" cha mwaka 1690 anasema kuwa;
"Mtu akifuata masharti yaliyowekwa na sheria anayo haki ya kurithisha mali zake kwa uhuru atakavyo yeye mwenyewe bila kuingiliwa na mtu yoyote".
Mwanafalsafa Hugo Grotius ameeleza dhana hii katika kitabu chake cha mwaka 1631 kiitwacho "The Jurisprudence of Holland". Dhana hii ya "Testamentary Freedom" inampa mzazi haki na huru wa kurithisha mali yake yote kwa mtu yoyote amtakaye hata kama ni mtu baki ambaye sio ndugu yake wa damu.
(iii) Msingi wa Kisheria wa Kunga ya Uhuru wa Kurithisha.
Katika Tanzania, msingi wa kisheria wa dhana ya Uhuru wa Kurithisha ni common law yaani hukumu za mahakama za Uingereza pamoja na Kifungu cha 46 cha the Indian Succession Act, 1865. Kifungu cha 46 kimpatia kila mtu akiwemo mzazi haki na uhuru wa kurithisha mali zake kupitia wosia kwa masharti kwamba mtu au mzazi huyo awe na akili timamu na awe na umri wa miaka 18 au zaidi. Tofauti na Sheria za Kiislam na Sheria za Mila, Sheria ya the Indian Succession Act, 1865 haijaweka sharti lolote kumlazimisha au kumshurutisha mzazi kurithisha mali zake kwa mke wake, watoto na ndugu wa damu bali sheria imempatia huru na haki ya kurithi mali zake na sheria hiko kimya kwenye swala la haki ya lazima ya mke na watoto wa marehemu kurithi za mali za marehemu mme au mzazi/baba.
Pale ambapo sheria ya Tanzania iko kimya au kuna pengo (lacuna) kuhusu swala lolote la kisheria basi tunaelekezwa kutumia Sheria za Uingereza (statutes of general application in England) au common law na Doctrine of Equity yaani Maamuzi wa Mahakama za Uingereza (Superior Courts) kama yalivyokuwa au kama sheria zilivyokuwa tarehe 22 July, 1920 na kurudi nyuma bila kikomo, hii ni kwa mujibu wa Kifungu cha 2 (3) cha sheria inayoitwa the Judicature and Application of Laws Act, Cap. 358 kama kilivyotafsiri na Mahakama ya Rufaa katika Kesi ya Issa Athman Tojo Vs Republic [2003] TLR 119. Kutokana na ukimya wa sheria ya the Indian Succession Act, 1865 kuhusu swala la haki ya lazima na ya moja kwa moja ya mke na watoto kurithi mali za marehemu mme au mzazi, basi ninalazimika kwenda Uingereza kutafuta sheria na uamuzi wa Mahakama za Uingereza kuhusu swala hili.
Kifungu cha 3 cha Sheria ya Wosia ya Uingereza ya 1837 (the Will Act, 1837) kinampa kila mtu akiwemo mzazi haki ya kurithisha mali zake kwa mtu yoyote amtakaye na chini ya kifungu hiki mzazi anaweza kumnyima urithi mtoto wake wa kumzaa au mke wake wa ndoa na kifungu hiki kinatumika Tanzania kwa sababu sheria ya Tanzania hiko kimya kwenye swala hili.
Kwa upande wa Common Law ya Uingereza, Jaji Mkuu wa Uingereza wa wakati huo, Mtukufu Cockburn mwaka 1870 katika kesi ya Banks v Goodfellow (1870) 5 LR QB 549 kuanzia ukrasa wa 563 mpaka 565 aliamua kuwa mzazi ana mamlaka yasiyokuwa na mipaka ya kurithisha mali zake kwa wosia na katika kesi hii Mahakama iliamua kuwa Wosia wa John Banks ni halali kisheria pamoja na kwamba ulimnyima urithi mtoto wake na badala yake kumrithisha mali yake yote kwa mpwa wake Margeret Goodfellow. Msingi mkuu au jurisprudensia ya kesi ya Banks v Goodfellow (1870) 5 LR QB 549 ilikuwa ni Kunga ya Uhuru wa Kurithisha Mali au Doctrine of Testamentary Freedom. Jaji Mkuu, Cockburn katika kesi ya Banks v Goodfellow (1870) 5 LR H.L. 549 katika ukrusa wa 563 alisema maneno yafuatayo:
"Sheria ya kila watu waliostaarabiki inakubali kuwa mmiliki wa mali anayo haki ya kuamua mtu gani amrithishe mali yake kupitia wosia wake wa mwisho. Na ni wazi kuwa sheria inampatia mmiliki wa mali huru usio kuwa na mipaka wa kurithisha mali zake kwa mtu amtakaye .......”