Je, ni halali kwa mgombea Urais CCM kufanya haya?

Nakupa Kudo's.
Hii kitu ndo nilikuwa naitafuta...!!!
 
..Ni rushwa ya wazi mkuu, Ila kwa mambo yalivyo nchii hii, na kwa sababu katiba yetu inampa madaraka makubwa sana raisi, ndo maana kuna umuhimu wa kufanya mabadiliko makubwa ya Katiba. Inatakiwa kusiwe na raisi kipindi hiki tunapoelekea uchaguzi mkuu, kwan raisi naye ni mgombea. Hii inapelekea kutumia urais wake kujijengea mazingira mazuri zaidi ya wagombea wengine ili kufanikisha ushindi
 
Kachanganyikiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ndugu yangu Mtanzania, Kama Kuna Uzalendo basi ni huu wa kukemea haya anayoyafanya huyu Mgombea wa Urais wa CCM....!!!
HATA KAMA ATASHINDA LAZIMA SHERIA ICHUKUE MKONDO KUMVUA USHINDI HUO...Hapashwi na hastahili kurudi Ikulu. No way!
 
Ndiyo maana tunawaangalia tu NEC wajifanye hawaoni Sasa na kwenye kura wajifanye pia hawajui matokeo mengine hata Kama watalindwa na vifaru tutawachomoa tu
Lissu atumie udhaifu huo kupiga spana zaidi!Maana NEC watahofia kumchukulia hatua huku wakimwacha JPM!
 
Maajabu na maigizo hayatoacha kuendelea bongoland,haya mataga njoon mtetee chama lenu chakavu huku
 
Ndiyo maana tunawaangalia tu NEC wajifanye hawaoni Sasa na kwenye kura wajifanye pia hawajui matokeo mengine hata Kama watalindwa na vifaru tutawachomoa tu

This time around lazima Wabongo WACHOMOE BETRI maaana hakuna namna....!!!
 
Kwanini Magufuli, CCM, NEC na TAKUKURU wanatufanya Watz hatuna akili? Hawa jamaa ni kuwa FYEKELEA MBALI ifikapo tarehe 28 Okt, 2020!

Mungu na atusaidie maana Tumechooooooooooka.
Refa wenu ni nani au BEBERU Amsterdam na ndiye atakayemtangaza Lissu?
 
Wanadai Amani Amani,Tuombee Amani,Tusivunje Amani ni tunu yetu!!!, Imeandikwa,"Hakuna AMANI kwa waovu,asema Bwana",Isaya 48:22
 
Tayari kuna barua hapa tunamalizia kuitype iende kwa wafanyakazi wa tume wamchukulie hatua za kukiuka kanuni za uchaguzi.
Japo inaweza isizae matunda ila lazima tuweke kumbukumbu sawa ili ikija tokea asiwepo wa kurahumu.
Afadhali iwe kweli kuwa kuna barua inaandikwa kwa sababu mambo ya hovyo yanayofanywa na Magufuli kinyume na taratibu ni vizuri yakawa documented kwa rejea za baadaye. Sheria na taratibu za Uchaguzi zanavunjwa waziwazi na Magufuli NEC wanakaa kimya tu bila hata kukemea tu kuwaaminisha watu kuwa hawako upande wa mgombea aliyewateua. Magufuli ni mtu asiyeelewa hata mambo ya msingi ambayo hata mtu wa kijiweni anayaelewa, kwa mfano inaonekana yeye anafikiri sababu ya Rais kubaki madarakani wakati wa kampeni ni ili asaidie Rais arudi madarakani, vivyo hivyo na Mawaziri ili warudi Serikalini. Bunge linavunjwa wakati huo ili wabunge warudi Majimboni kwao kupisha bunge jipya Serikali na Mahakama zinabaki ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma walizozoea mpaka Serikali mpya iapishwe. Kwa hiyo ni kosa na ni rushwa kutumia fedha za Umma kupeleka miradi mipya kwa wapiga kura wakati wa kampeini hata kama Rais angekuwa siyo mgombea. Bahati mbaya sana kwa uchu wa kubaki chama tawala, hata Chama chake wanakaa kimya bila kumshauri ajiepushe
na vitendo vya kumharibia yeye na Chama pia. Wagombea wanatakiwa wafanye kampeini zao kwenye mazingira sawa kuleta matokeo chanya.
 
Refa wenu ni nani au BEBERU Amsterdam na ndiye atakayemtangaza Lissu?

Refa anayependelea timu mojawapo ni hatari kuliko Beberu la Mbuzi! Huu ujinga wa kumwita BEBERU kila mtu anayem- challenge Magufuli hakika ni ulimbukeni na ujinga kiwango cha lami!!
 
Serikali haiko likizo jua hilo. Kuna mhimili mmoja umejichimbia mizizi zaidi. JPM ni muwazi kupitiliza hayo yote alisha waambieni huko nyuma. Tatizo wengine muwagumu mno kuelewa.
 
Hicho kipengele cha sheria ulichokiweka hapo kinamzungumzia Waziri kutotoa ahadi lakini na wao hawajafanya hivyo bali anayetoa ahadi na kuamuru shughuli hizo zifanywe ni Rais ambaye anayo mamlaka kikatiba kufanya hivyo, kwa hiyo mleta hoja usipotoshe ukweli wa kisheria, ingekuwa Waziri ndo kaamuru shughuli hizo kufanywa hapo ungekuwa na hoja. Lakini kwa mimi naona kunatakiwa kufanyike mabadiliko ya sheria ili hata Rais aliyepo madarakani na anagombea inapofika kipindi cha kampeni basi asijihusishe na kuamuru kufanywa shughuli zozote za maendeleo bali kazi hizo zifanywe na Watendaji wengine wa Serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…