Je ni ipi adhabu ya mdhamini wa kifungo cha nje?

jerryempire

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2017
Posts
5,530
Reaction score
9,550
Habari,
Naomba kujua adhabu kwa mdhamini ambaye amemchukulia mtu dhamana baada ya kufungwa kifungo cha nje.

1,endapo mtuhumiwa atakimbia?
2,endapo mtuhumiwa hatokuwa anakwenda kufanya usafi kwa wakati.?

na je kama mdhamini atafanikiwa kumchukua mfungwa wa nje na kwenda kumkabidhi mahakamani na kujitoa udhamini je inaruhusiwa kisheria?

maana kabla ya hukumu mtuhumiwa alitolewa dhamana na dhamana yake ilikuwa ya bondi ya shilingi laki 3,Lakini baada ya kufungwa akatolewa gerezani na kufungwa kifungo cha nje lakini mara hii dhamana yake haikuandikwa ni shilingi ngapi bali endapo mtuhumiwa atatoroka basi tunatakiwa kushirikiana kumpata mtuhumiwa,sasa hapo sijaelewa itaplay ile ile laki 3 au ndo kwenda jela tena.

na je kesi kama hizi huwa zinaisha kumalizwa kimya kimya au ndo mpka mtu amalize hukumj yake?

Ahsanten
 
Mfungwa hana dhamana, ndio nakusikia wewe leo kwa Mara ya kwanza.

Anayedhaminiwa mahakamani ni mahabusu tu ambaye kesi yake bado IPO mahakamani.
 
Kama ametoka au kawekwa kifungo cha nje under Community Service Act No 6 ya 2002 iliyofanyiwa marekebisho 2004 mdhamini yupo. Hapa hakuna gharama wala bond kikubwa mdhamini huyu awe na makazi ya kudumu. Endapo mfungwa wa Community Service atatoroka atatakiwa kutoa ushirikiano kwa probation officer wa sehemu husika ambae atapelekea details za mfungwa huyo polisi ili aweze kupatikana. Pia mdhamini anaweza kujitoka kikubwa apeleke taarifa hiyo mapema kwenye ofisi za probation and Community Service za sehemu husika.
 
Mfungwa hana dhamana, ndio nakusikia wewe leo kwa Mara ya kwanza.

Anayedhaminiwa mahakamani ni mahabusu tu ambaye kesi yake bado IPO mahakamani.

Kapitie sheria ya Community Service no 6 ya 2002 uone vigezo na masharti vya mtu kupata kifungo hichi
 
Mfungwa hana dhamana, ndio nakusikia wewe leo kwa Mara ya kwanza.

Anayedhaminiwa mahakamani ni mahabusu tu ambaye kesi yake bado IPO mahakamani.
mfungwa wa kifungo cha nje anakuwa na wadhamini wawili ambaye anakuwa anafanya community services
 
Back
Top Bottom