Je, ni jukumu la nani?

Je, ni jukumu la nani?

bombu

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2011
Posts
1,127
Reaction score
542
Katika jamii nyingi za kiafrika hususani Tanzania, mwanaume ndiye huanzisha mahusiano kwa kumtongoza binti na hata kumchumbia kwa lengo la kuwa pamoja. Sasa inapotokea mwanaume/kijana akamtongoza binti bila kuweka bayana iwapo ana nia ya kumchumbia namaanisha anamuomba wawe wapenzi, na binti akaridhia (akiamini kuwa uchumba utafuata), na katika mahusiano hayo ukapita muda mrefu wa labda hadi miaka mitatu na kuendelea bila kijana wa kiume kutamka uchumba au nia ya kufunga ndoa.

Na katika mahusiano huui wawili hujikuta wanapata m/watoto na mwanamke huonekana kama hakuwa thabiti kwa kukubali kazaa na mtu ambaye hawajafunga ndoa (mtazamo wa jamii). Je, ni jukumu la nani kuhakikisha kuwa panakuwepo uhalalishwaji wa mahusiano (ndoa) kati ya mtu mume na mtu mke?
 
Mi nadhani ni jukumu la mwanamke kuweka msisitizo kwa mwanaume ila wahalalishe hyo ndoa. Wanaume ni watu ambao mara nyingi ( sio wote) hawajali.
 
Katika jamii nyingi za kiafrika hususani Tanzania, mwanaume ndiye huanzisha mahusiano kwa kumtongoza binti na hata kumchumbia kwa lengo la kuwa pamoja. Sasa inapotokea mwanaume/kijana akamtongoza binti bila kuweka bayana iwapo ana nia ya kumchumbia namaanisha anamuomba wawe wapenzi, na binti akaridhia (akiamini kuwa uchumba utafuata), na katika mahusiano hayo ukapita muda mrefu wa labda hadi miaka mitatu na kuendelea bila kijana wa kiume kutamka uchumba au nia ya kufunga ndoa.

Na katika mahusiano huui wawili hujikuta wanapata m/watoto na mwanamke huonekana kama hakuwa thabiti kwa kukubali kazaa na mtu ambaye hawajafunga ndoa (mtazamo wa jamii). Je, ni jukumu la nani kuhakikisha kuwa panakuwepo uhalalishwaji wa mahusiano (ndoa) kati ya mtu mume na mtu mke?

Jukumu ni la Mwenye Shida, la sivyo mwanamke akubali sera ya mfumo dume!
 
asilimia kubwa ya ndoa hufungwa kwa shinikizo la wanawake husika ktk mahusiano husika. Mwanamke ukilemaa ukitegemea 'hisani' ya ndoa, weeeeeeeeee, utamegwa mpaka uchoke ukishtuka analetwa mwenzio kisha ndoa then unabakia oooooooooh kanitumia then kaniacha!
 
Back
Top Bottom