Nimewahi kuagiza kupitia Beforward mara tatu mimi binafsi na mara mbili niliwasaidia jamaa zangu. Wako vizuri sana. Tatizo la watu wengi wanaangalia bei. ukiona gari lina bei rahisi ujue ni la zamani zaidi au limetembea Km. nyingi.
Pia unavyoangalia picha za gari chunguza zaidi na unaweza kuwaomba wakutumie picha kwa sehemu ambayo una mashaka nayo. Mara nyingine picha zao huonesha na sehemu yenye hitlafu hasa katika body. Kwa ujumla picha zao sio fake. Pia unaweza ku-negotiate bei.
Kuna jamaa yangu pia aliwahi kuchagua gari kwenye mtandao, na alipoliagiza baada ya ukaguzi akaambiwa gari hilo halifai. Maana yangu magari yao hukaguliwa kwa umakini zaidi ingawa hata makampuni mengine hukaguliwa ili gari linaloingia nchini liwe katika kiwango kinachokubalika.
Unaweza kupata gari lako ndani ya mwezi mmoja kulingana na ratiba ya meli. Movement zote unapata mtandaoni, tangu siku wanayofanya ukaguzi, linavyopakiliwa melini, siku ya kuondoka na siku ya kufika mara nyingi tangu meli iondoke bandarini ni siku 21.
Sijajaribu makampuni mengine kwani nimeridhika na hawa jamaa.