Je,ni kawaida kuingia hedhi wakati unanyonyesha?

Kolis

Member
Joined
Dec 13, 2012
Posts
35
Reaction score
2
Habari zenu wakuu? Nijambo la kawaida kweli kupata hedhi ukiwa unanyonyesha?kama sio ni dalili ya nini? Naomba mnieleweshe. Natanguliza shukrani.
 
Hedhi haihusiani na kunyonyesha, kupata hedhi wakat unanyonyesha ni jambo kawaida
 
Habari zenu wakuu? Nijambo la kawaida kweli kupata hedhi ukiwa unanyonyesha?kama sio ni dalili ya nini? Naomba mnieleweshe. Natanguliza shukrani.
Kolis, wakati wa kunyonyesha sio wote ambao hawapati hedhi, kutopata hedhi wakati wa kunyonyesha inaitwa lactational amenorrhea na husababishwa na wingi wa kichocheo kinachoitwa Prolactin ambayo ndiyo inayosababisha kutoka maziwa, husababisha kuwa kukosa hedhi, kupata hedhi ukiwa unanyonyesha haina madhara yoyote.
 
Last edited by a moderator:
Shukrani sana mkuu,kumbe iko kitaalam kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Ni kawaida, wamama wengi huanza pata hedhi baada ya siku 40 tangu kujifungu, wengine miezi 3, 6 .... ila wengine ni mpaka wamalize kunyonyesha!
 
Si kwamba ni kawaida tu, mwanamke anatarajiwa apate hedhi kila mwezi isipokua miezi ya ujauzito tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…