Je, ni kiswahili fasaha kusema 'Mvua za El Niño'? Kwani hizi mvua ziko ngapi?

secretarybird

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2024
Posts
23,984
Reaction score
51,055
Kwenye taarifa ya habari utasikia "Mvua El Niño", kwenye vijiwe utasikia "mvua El Niño".

Kwani hizi mvua ziko ngapi?

Hata juzi nimesikia wataalamu wa Kiswahili kutoka BAKITA nao wakisema "mvua za El Niño".

Je, kati ya mvua El Niño, na mvua za El Niño ipi sahihi?
 
Hata watu wa BAKITA wamenishangaza kwa kusema 'mvua hizi'.

Siku mmoja mtu atasema hizi maji na watu wataona tu vema.
Wapo sahihi Wala hawajakosea MVUA HIZI hapo wakimaanisha Kuna mvua zitajitokeza za aina nyingi kwa kipindi hiki🙏au ulitaka waseme mvua hii wakati ni mvua zenye mabadiliko
 
'Mvua za El nino' ndiyo sahihi kwa sababu kipindi chote cha masika, mvua nyingi hunyesha, hainyeshi mvua moja tu.
 
Wapo sahihi Wala hawajakosea MVUA HIZI hapo wakimaanisha Kuna mvua zitajitokeza za aina nyingi kwa kipindi hiki🙏au ulitaka waseme mvua hii wakati ni mvua zenye mabadiliko
Hapo napinga. Mvua ni nomini isiyo na idadi/ isiyohesabika. Ni kama maji tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…