Primary school nilikua na vichekesho sana mpaka namaliza la saba halaf nilikua sinaga akili. Vichekesho vilinipa umaarufu sana.
Secondary nilikua serious nikawa napiga sana misuli, nilikuaga top 3 mpaka naondoka form 4 na one kali. Akili zininifanya kuwa maarufu sana.
High school nilikuaga mkarimu sana, maana Boarding school ilikua mkoani kwetu hivyo mamaa na ndugu zangu walikua wanakuja sana kunitembelea na kuniletea mazaga, tranka yangu ilikua ni ta room members woote. Wakija wazee na mazaga ilikuaga bata kwemda mbele hata watu wa room zingine walikua wanakuja kwetu.
Nakumbuka graduation ya form 6 mama na mzee waliandaa party ya jamaa zangu woote wanne kwakua wao walikua wanatokea mikoa ya mbali. Ukarimu ulinifanya wengi kunifahamu , "aahh yule jamaa peace sanaa" ndio msemo uliokua unanitambulisha shulen