FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 38,920
- 44,970
Teknolojia hii inayohusisha kupandikiza kifaa kidogo mfano wa shillingi ndani ya fuvu ambapo viwaya vyembamba mara laki ya unene wa nywele, huchomekwa nankuungwa na neurons za ubongo, itawezesha binadamu kuzunguza kuwasiliana bila kufungua mdomo (sauti) wala kuandika (herufi). Teknolojia hii itawezesha watu kuendesha magari bila kushika usukani, kupiga simu bila kuwa na simu mkononi. Itawezesha kucheza game bila kushika contol, kubadilisha channel za Tv bila kushika remote control, kuwasha taa bila kubonyeza switch. Kuhamisha pesa bila kushika ATM kadi nk.
Hii inawezekana vipi? Ni kwamba utakuwa unaamrisha mifumo ya kidijitali kwa kuwaza tu (wireless transmission), yaani ukiwaza gari liwake, basi linawaka, ukiwaza taa ziwake, zinawaka, ukiwaza TV iwake , inawaka, ukiwaza unampigia simu nduguyo aliye marekani, hapo hapo unaanza kuongea nae, kwa kuwaza tu.
Watu wenye ulemavu wa kuparalyse watatembea, maana miguu yake itaendeshwa wirelessly kwa kutumia bypass ya Neuralink, vipofu wataona, nk, nk. Utaweza kudownload kumbukumbu zako zote na kuzisave kwenye backup server, na ukitaka kuzirestore unazirudisha endapo umesahau, au ukitaka unaweza kuinstall kumbukumbu zako kwenye ubongo wa mtu mwingine, mfano proffessor wa hisabati anaweza kudownload memory zake na kuziinstall kwenye ubongo wa mwanafunzi wake, na akawa proffessor ghafla!!!
Tayari mambo yameanza kuiva, kifaa hiki alifungiwa nyani miezi michache iliyopita, na akaweza kucheza game aina ya ‘mindpong’ bila kushika Joy stick, yaani aliicheza game kwa kuwaza tu. Nyani mwenyewe ndio huyo hapo chini.
INTERNET OF THINGS itaunganisha kila kitu na bongo za kila mtu na kuwa one consiousness, Fahamu moja, as if ni kiumbe kimoja!
=========================
Update: 27/05/2023
===========================
Update: 30/01/2024
View: https://www.instagram.com/p/C2uvtC5sM4n/?igsh=NTc4MTIwNjQ2YQ==