Je, ni kwanini Utajiri wa Mtanzania (Muafrica) hauna muendelezo?

Je, ni kwanini Utajiri wa Mtanzania (Muafrica) hauna muendelezo?

Megalodon

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,534
Reaction score
7,866
Kwa sasa Utajiri wa nchi na wafanyabiashara wakubwa na wanaotambulika RASMI upo chini ya wasomali, wahindi na waarabu!

Rarely au hakuna kabisa kumkuta Mtanzania amepenya hapa.

Kama Mtanzania akifanikiwa kuwekeza na akafika angle fulani ya kuwa na UTAJIRI RASMI kisha ikitokea amefariki, basi kwa asimilia kubwa habari ndio imeishia hapo; hii ni tofauti na wenzetu wahindi, waarabu na wasomali?

Shida huwa ni nini?

Kwa mfano, Kuna kipindi the Late Reginald, alikuwa na utajiri unatambulika Rasmi, baada ya kifo chake habari ya Utajiri iliishia hapo.

Kilichofuata ni kushinda mahakamani, familia kutishiana uhai, mali za MENGI nyingi sana zimeshanunuliwa ikiwemo maji ya kilimanjaro na kwa sasa ITV ipo kwenye final stage ya kupigwa sale, mnunuzi anaweza kuwa bakhresa na hato badili jina kama ilivyokuwa kwa maji ya KILIMANJARO. Kwa sasa maji ya Kilimanjaro unanunua kwa 500 yale lita moja.

Reginald is like he never existed ? Hii kitu ni ngumu kwa wasomali, waarabu na wahindi they have what it called CONTINUITY!

Je, sisi ngozi NYEUSI shida ni nini?

Tupeane mawazo, tunakwama wapi kwenye business CONTINUITY.

Kwanini NGOZI nyeusi mtoto anaanzia chini , baba anaanzia chini, mjukuu anaanzia chini. wanaanzia chini, while kwa Wasomali, Waarabu na Wahindi, watoto wanaanzia alipoishia baba. Wajukuu nao wananzia alipoishia baba ….. list goes on

What is wrong with us?
 
Utajiri kwa nchi zetu hizi ni siri ya mtu wakati kwa hao wenzetu uliowataja ni siri ya Familia husika na hata Kama sio Familia nzima basi wapo watu wanafahamu nini kinafanyika.
Mkoa nilipo wapo wahindi na waarabu wao biashara ndio maisha yao. Kijana akifikisha umri wa shule ataenda hadi kidato cha nne labda na baada ya hapo atapelekwa chuo akasome certificate au diploma ya biashara. Akirudi anapewa ofisi au kitengo cha kusimamia na mambo yanakuwa hivyo.

Africans Sasa Kama
Sauli ni yeye tu
Nganga ni yeye tu
Widambe ni yeye tu
Champion ni yeye kama yeye

Utajiri ni SIRI SANA.
 
Mzazi wa kiafrika anataka mtoto wake asote kama yeye alivyosota, kiufupi waafrika wamefanana Kwa 90% na wanyamapori.

Kama nimewakosea mnisamehe.
 
Sababu ni nyingi kwa experience yangu tatizo ni
1. Kutowashirikisha watoto katika biashara hivyo wanakuwa hawajui waanzie wapi
2. Kumwambia mtoto/watoto kuwa hii siyo mali zake atafute za kwake
3. Kutaka watoto wako waajiliwe na serikali badala kwenye biashara zako
4. Extended family
5. Kutoteua mtoto msimamizi wa mali ungali mzima
6. Masuala ya ndoa kuoa ovyoovyo mwanamke usiyemfahamu
7. Kutawanyika badala ya kuishi pamoja
8. Kugawana mali badala ya kuziendeleza
9. Starehe
 
Hatuwaendelezi watoto katika yale tunayoyafanya, hao waarabu watoto wao wanasomea biashara, nenda kwenye vyuo vya biashara utakuka idadi yao ni kubwa, akishasoma anaenda kuendeleza kile mzazi wake ameanzisha, sisi sasa Baba ni fundi selemara mtoto anaenda kusomea public health wapi alichokianzisha baba kikaendelea utajiri utaendelea wapi?

Pili utajiri wa Mwafrika ni fake, unatumia nguvu za giza zaidi sasa kurithisha utajiri wa namna hiyo ni ngumu kuurith, ndio maana utaona matajiri wa mabasi wakifa na biashara zao zinakufa
 
Back
Top Bottom