Moja kati ya jambo lililofanikiwa kwa kiwango kikubwa katika uongozi wa awamu ya sita ni kuimarisha Diplomasia ya nchi yetu na kurejesha nafasi ya Tanzania katika mawanda ya diplomasia Duniani. Rais Samia anastahili "honoris causa" katika hili. Tuangazie baadhi ya faida za kuimarisha Diplomasia na ushirikiano wa kimataifa kwa Tanzania:
Mkuu Nyabukika, Maoni yako yabaheshimika....Usipotoshe.
Diplomasia, kiuhalisia, umekuwepo enzi na enzi....utani au mila na jadi zetu kuwa na Watani ni Diplomasia.
Kitu kikubwa katika Diplomasia ni kuheshimu mipaka ya nchi(sovereign state) na ndio maana kuna itifaki za kuongoza kuheshimiana kwa kuhakikisha mila na jadi hazikanyagwi...ndio maana balozi anapewa credentials... Watani vilevile walipewa mpaka wake... na hili tena limenikumbusha stori ya barua aliyopata Speke wakati akitafuta njia za kwenda kwa 'Wangwana' mimi natambua stori hiyo ni Diplomasia ya aina yake hivyo basi hata wangwana pamoja na kuwa na bifu na Sultani, waliheshimu mipaka yake na kumpatia ushirikiano bwana Speke....historia inajieleza tunajua yaliyofuata na kujiri baada ya hapo...ni muhimu kuheshimu mipaka na kutokuvukua.
1. Diplomasia inafungua milango kwa wawekezaji wa kimataifa na wafanyabiashara wakubwa kuja nchini kwetu. Katika kipindi cha miaka miwili tunaona namna TIC inavyozidi kusajili wawekezaji wengi.
Hayo juu yamekuwa ni malengo ya miaka karibia miaka 144 iliyopita, haijalishi waheshimu tu Sheria zetu, mila na jadi zetu, yaani Tamaduni zetu kwa ujumla Kwani tatizo limekuwa wao kutaka kufanya walitakalo. (interfering with our sovereign state) bila ya kujali mila na jadi zetu, miongozo yetu, Sheria zetu.
2. Diplomasia inafungua milango kwa Taasisi mbalimbali za kimataifa kufanya kazi na serikali yetu katika nyanja za kiuchumi na maeneo mengine ya kijamii kama vile huduma za Afya
Hakika na ulichosema, "inafungulia milango" Mwanzoni walianza na Biashara, Dini, na Huduma za Afya... hivyo basi, hakuna kikubwa watakacho kileta kwani tulishajitosheleza katika hizo nyanja, za kiuchumi na kijamii mengine ni ziada na hakuna kosa la kujifunza mengine....tunaona athari, manufaa n.k katika ufunguaji wa Milango Lakini wasitumie njia na nyanja hizo kutufubaza na kutuhadaa....historia isijirudie
.
3. Diplomasia inafungua soko la bidhaa za Tanzania kwa mataifa mengine na kuchochea ukuaji wa hifadhi ya fedha za kigeni nchini. Hii ina maana kubwa katika uchumi wetu.
Ni ulimbukeni tu, bidhaa zetu zimekuwa na soko enzi na enzi, hayo ya Fedha za kigeni ni utumwa tuu.
Kwa miaka mingi imekuwa hoja zetu kuwa hizo nchi Duniani ndio wafungue milango na soko la bidhaa zetu ziwanufaishe Wananchi wetu, na sio tuwafungulie milango wachote na kujinufaisha wao tu
Mkuu, dhana uliyoiweka ni kama vile kusema tumekuwa tumefunga milango wakati huo sio Ukweli.
We would like and prefer a revolving door?
Mpe pongezi Raisi, lakini ukumbuke kuwa na yeye ameapa kulinda mipaka na sheria za nchi yetu. Hivyo basi na kwa mantiki hiyo, hao madiplomat wansopewa ridhaa na Raisi wetu, waheshimu mipaka na sheria za nchi yetu.
Jioni njema.