Kabla ya mwaka 1885 Deutsch-Ost Afrika au Tanganyika hazikuwepo.
Wapelelezi wa Kijerumani waliosaini mikataba na machifu ni Dr Karl Peters na Dr Karl Juhlke.
Maeneo mengi ya huku Tanzani bara yalikuwa chini ya usimamizi wa Zanzibar (Under Suzerainity).
Sehemu kama Arusha (Aruscha) na Kilimanjaro zilikuwa ziko chini ya Sultan wa Zanzibar ambaye naye aliwadanganya machifu wa huku bara. Tatizo lilianza ni kwamba Dr Karl Peters na Dr Karl Juhlke waliwashinda waarabu akili. Wenyewe walienda kusaini mikataba mipya na machifu wa huku bara ambapo, hao machifu walisema hawako chini ya Sultan. Aliyewasaidia wakina Karl Peters kumzunguka Sultan alikuwa ni mwarabu na Mkalimani Bwana Ramadhani ambaye alitumika kama mtafasiri aliyesaidia kusainiwa mikataba feki.
Kipindi hiki pia, Sultan wa Zanzibar alikuwa na ofisi ya kibalozi huku bara. Msimamizi wa hii ofisi alisema wazi kwamba Sultan hakuwa anamiliki maeneo yoyote huku bara mbali na maeneo ya Pwani. Baada ya mkutano wa Berlin kuisha mwaka 1884, Sultan wa Zanzibar aliandika barua kwa Mfalme wa Ujerumani na Uingereza, kwanini walimzunguka na hakushirikishwa ilhali maeneo mengi ya huku bara ni yake. Sultan wa Zanzibar alifanya makubaliano mengine kuhusu Mombasa, kipindi hicho akimshirikisha Muingereza na Mjerumani.
Taarifa hizi kuhusu maeneo ya kule Kaskazini na Sultan kutaka kuyatawala, mara ya kwanza kabisa ziliwekwa wazi mwaka 1972 na Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania. Wanasheria na watafiti wa Wizara, Bwana Earl Seaton na Sosthenes Maliti waliandaa chapisho zuri kabisa ambalo liliweka wazi hii mikataba na barua za Sultan kwa wafalme wa Uingereza na Ujerumani kuhusu maeneo ya Tanganyika. Kiufupi, hao wanaoshabikia usultan kwasababu za kidini huwa nawaona kama watu fulani waliopagawa akili.
Nikipata wasaa ntayaweka hayo machapisho na zile barua, nadhani bado zitakuwepo kwenye ile maktaba. Kuna machapisho yanaitwa Tanzania Treaty Series, yalikuwa yanaandaliwa na Foreign Affairs Office, lakini waliacha kuyachapisha. Mle ndani hadi mikataba yote kuhusu Tanganyika mnamo karne za 19 na 20 mwanzoni ipo.