KWELI Je, ni kweli hao ni bodaboda kutoka jijini Dar es Salaam?

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Kumeibuka video inayosambazwa kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) ikionyesha idadi kubwa ya waendesha bodaboda wakiwa barabarani wakitekeleza shughuli zao za kawaida.

Mojawapo ya machapisho yanayosambaza video hiyo linadai kuwa watu wanao onekana ni maafisa wa usafirishaji wanaofanya kazi katika Jiji la Dar es Salaam.
je ni upi uhalisia wa chapisho hilo ?



Your browser is not able to display this video.
 
Tunachokijua
Je, ni video hiyo imerekodiwa wapi?

Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia Google Reverse Image Search umebaini video hiyo ilichapishwa na vyanzo mbalimbali ambapo Juni 21, 2026 ukurasa unaotumia jina la @cosmashaule720 katika mtandao wa TikTok ulichapisha video hiyo pasipo maelezo yoyote, lakini baadhi ya waliotoa maoni wanaeleza kuwa eneo hilo ni Veta Dar es salaam.

Kadhalika kupitia chapisho la JamiiCheck baadhi ya wadau wametaja pia kuwa eneo hilo ni Veta huku wengine wakitaja kuwa ni makutano ya barabara Chang'ombe Dar es salaam.

Aidha namba za usajili wa pikipiki (boda boda) Zinaanza na "MC" (kama vile MC 7** FKM na MC 2** FJP), ambapo ni muundo wa usajili wa pikipiki nchini Tanzania. Kadhalika baadhi ya waendesha pikipiki wanaonekana wakiwa wamevaa kofia ngumu (Helmet) kutoka kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) ambazo zimekuwa zikitumiwa na baadhi ya watanzania ikiwemo wakazi wa Dar es Salaam.

Aidha kupitia Google Earth inaonesha muonekano wa eneo hilo ambalo ni 'chang'ombe flyover' ambalo muundo wa daraja, majengo yanayoonekana vyote vinafanana na mazingira yanayoonekana kwenye video hiyo.​
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…