Je, ni kweli huduma za afya zimeboreshwa?

Je, ni kweli huduma za afya zimeboreshwa?

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Rais Samia Suluhu anaendelea kuboresha sekta muhimu zinazomlenga direct mwananchi na sekta ya afya aliipa kipaumbele, Serikali ilitenga bajeti katika sekta ya afya shilingi Trillion 1.1 ili kukamilisha mahitaji yote yanayotakiwa katika sekta hiyo ikiwemo ununuzi wa vifaa tiba, ujenzi wa vituo vya afya nk.

Lakini Rais Samia Suluhu aliona haitoshi kwa kujali kwake afya za wananchi wake aliongeza kiasi cha Tsh Bilioni 891.5 na tukafanikiwa kununua CT SCAN 34 ambazo zilipelekwa mikoa yote Tanzania hapo awali kulikua na CT SCAN 2 tu Tanzania nzima.

Lakini pia amefanikisha ununuzi wa magari ya wagonjwa (AMBULANCE) 720 na yamesambazwa wilaya zote Tanzania na magari haya yatasaidia kurahisisha usafiri kwa wagonjwa na kupunguza vifo vitokanavyo na kuchelewa kufika sehemu ya kutolea huduma.

Rais Samia Suluhu amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuboresha sekta ya afya mpaka vijijini sasa haina haja ya kwenda mjini ili upate matibabu.
 
Back
Top Bottom