Je, ni kweli Iddi Amin alikusanya walemavu na kwenda kuwamwaga Mto Nile?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Kwa yanayoendelea Congo nimebaini kuwa vita zina propaganda nyingi sana. Kwenye historia ya Idd Amina tumeambiwa kwamba Iddi Amin akiwa Rais aliwahi kufokewa na mlemavu kwamba ameshindwa kuiongoza Uganda. Siku chache zijazo Dikteta alikusanya walemavu wote mijini wakaenda kumwagwa wote mto Nile kuliwa na mambo.
Hii stori ni ya kweli?
 
Hapo uliposema walemavu WOTE ndo uongo. Mengine sijui.
 
Hakuna ushahidi ila ni ukweli kuwa iddi amini alihusishwa na ukiukwaji wa haki za binaadamu.
 
Kwa yanayoendelea Congo nimebaini kuwa vita zina propaganda nyingi sana. Kwenye historia ya Idd Amina tumeambiwa kwamba Iddi Amin akiwa Rais aliwahi kufokewa na mlemavu kwamba ameshindwa kuiongoza Uganda. Siku chache zijazo Dikteta alikusanya walemavu wote mijini wakaenda kumwagwa wote mto Nile kuliwa na mambo.
Hii stori ni ya kweli?
Nyerere alikua bingwa wa propaganda ni propagandist mzuri kwa madui wake wa kisiasa mgambo wakati mchakamcka walikua wanaimba kambona kakimbia ulaya kuolewa.........kwasababu kambona alimpinga Nyerere wazi wazi.
 
JamiiForums1945630163.jpg
 
Propaganda za Mzee Mchonga
Siyo propaganda za Nyerere.
Aliwakorofisha wakoloni wake wa zamani, akamgusa na myahudi hapo ndipo alipokosea.
Hao jamaa wakikusudia kumchafua mtu au kumuundia zengwe anaonekana mtu katili, wa hovyo, muhalifu na hafai kuishi duniani.
Unafikiri kazi za BBC, CNN, VoA, France24, DW na vingine ni nini?
Jibu propaganda tools.
 
Ukiwa ndani ya Uganda Idd Amin ni mtu aliyekuwa anapendwa sana na hata ukimuuliza mganda yoyote hawezi kukubali haya matope aliyopakaziwa. Idd Amin hajawahi kula nyama za watu bali kilichomponza huyu marehemu ni kutaka kuimega ardhi ya Tanzania. Jambo lingine alitengeneza uadui na mataifa ya magharibi, kuwanyang'anya wahindi maduka yao na kujenga urafiki na mataifa ya kiarabu akina Libya na wengineo
 
Mchaka Mchaka shule ya msingi kipindi hiko tulikua tunaimba...

🎶Idd Amini akifaa
Mimi siwezi kulia
Nitamtupa kagera
Awe chakula Cha mamba🎶🎶
 
Iddi amini ali wakata vipande watoto wake akaweka kwenye friji 😅😅propaganda za kindezi sana hizi zilikuwa
 
Nyerere alikua bingwa wa propaganda ni propagandist mzuri kwa madui wake wa kisiasa mgambo wakati mchakamcka walikua wanaimba kambona kakimbia ulaya kuolewa.........kwasababu kambona alimpinga Nyerere wazi wazi.
Nyerere alikuwa Mtunzi wa Nyimbo ?!!!

Au hizi ndio Propaganda zenyewe shortcomings zako unamsingizia Nyerere....
 
Back
Top Bottom