Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out!

Mungu hajaribiwi wala hadhihakiwi nimekutoa utumwani (jalalani) hadi kwenye utukufu ukiniudhi nitakurudisha makunyambani.
 
Wamuongeze Maliyamungu ana miss press conference kila siku....hajazoea wewe Ummy wewe ....jiangalie ! Wore mko sawa mbele Iwe
 
Hivi wajameni hii siyo taarifa ya status ya ugonjwa wa Corona na wala sio update ya Corona, hili ni angalizo la swali nimeuliza na alama kabisa ya kuuliza! Mimi mwenzenu kazi yangu ni kuuliza tuu maswali,
Sasa unavotuuliza sisi unatutafuta nini sisi mkuu... wenye mamlaka na maswala ya korona unawajua ksbisa. Usituingize mtegoni 😓😓😓
 

Hakuna kitu ambacho kitanifurahisha kama kuondoka madarakani kwa CCM na serikali ya mapinduzi zanizbar, bahati mbaya kwa hali ilivyo nchini tanzania hilo haliko karibu kutokea karibuni. Kwa hiyo i hope nitakukumbuke lakini kwa muda mchache ujao, usijidanganye ndugu yangu.

Mabadiliko ya Tanzania yatabadilishwa na watanzania wenyewe lakini kwa masikitiko mengi watanzania hawawezi hilo kwa sababu ni watu wa maneno mengi ila hatuna vitendo na tena ni waoga sana.
 

Hakuna watu waoga ni wakati utawaamsha

CCM wanaondoka bila kutegemea soon
 
Salama Aboud Talib (Waziri wa Nishati - SMZ) ashukiwa kuugua CORONA.
************************************************************************
Waziri wa Nishati wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ambae alikuwa safarini kutokea London (Uingereza [emoji636]) na kupitia Italy [emoji634] kisha kurejea Zanzibar wiki tatu zilizopita, amelazwa katika hospitali ya Mnazi mmoja akiwa katika hali mbaya huku akishukiwa kuwa ana maambukizi ya virusi vya CORONA...

Dr. Mkuu wa Hospitali ya mnazi mmoja baada ya kumpima vipimo vya awali na kutokana na dalili alizonazo mgonjwa huyo, aliamuru mgonjwa huyo kupelekwa katika eneo maalum la uangilizi kwa ajili ya wagonjwa wote wenye virusi vya corona, lakini Waziri huyo aligoma kuondoka katika Hospitali ya Mnazi mmoja akiwaeleza madaktari kuwa yeye kutokana na hadhi yake ya Uwaziri hastahiki kwenda kulazwa katika Hospitali ya Kidimni...

Mmoja wa wauguzi anaemshughulikia Waziri huyo amesema, Waziri huyo alipokelewa jana akiwa hali tete, huku akichuruzikwa na wingi wa mafua na kikohozi kisichonyamazika... Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa na dalili zote za virusi vya CORONA 🦠...

Hali hiyo imepelekea wauguzi na madaktari kuwa katika wakati mgumu huku kila mmoja akikhofia kuambukizwa ugonjwa huo na kuweza kuenea kwa watu wengine, kwa kile kilichotajwa kuwa mbali ya kugoma kwenda Kidimni, lakini pia Waziri huyo amegoma kuvaa mask na vifaa vyengine vya kudhibiti kueneza virusi vya CORONA anavyoshukiwa kuathirika navyo kutokana na Safari yake ya London kisha kupitia Italy na kurejea Zanzibar akiwa na homa kali!...

Mmoja wa wauguzi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja alisema amesikitishwa sana na kitendo cha Waziri huyo kugoma kupelekwa kwenye kituo cha uangalizi, huku Serikali ikimfumbia macho kwa sababu tu ya cheo chake...

Muuguzi huyo alisema kuwa licha ya taarifa hiyo kupelekwa kwa Waziri wa Afya hadi sasa, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa, na mgonjwa huyo bado yupo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja pasi na kuvishwa vifaa vya kuzuia maambukizi yasienee kwa wengine...

Kutokana na taharuki hiyo, muuguzi huyo ameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuacha UBAGUZI katika mambo ya msingi yanayoweza kuhatarisha maisha ya Wazanzibar wote!... Ameitaka SMZ kupitia Wizara ya Afya kuhakikisha mgonjwa huyo anaondoshwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kama ilivyofanyika kwa wagonjwa wengine ili kuepusha kuenea kwa haraka maambukizi ya ugonjwa huo hatari!...
 
Mbona unaleta kitu cha tangu Jmapili mkuu na paschal mayala alishakileta? Umetoka usingizini??
 
Aache ungese
 
Wamuache Afe tu mbona simple jitu lina korona kisa waziri ndio akae kingese nashauri kama bado yupo wauguzi wasimsogelee siku mbili hizi tuone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…