Je ni kweli kuwa anayejua Baba wa Mtoto ni Mama?


Sure!
Na hiyo ni kali sana,Manake mtoto akitoka hapo ni kijoti kuliko joti orijino.
 
mbona kitu ni kile kile, kama mwanaume ni yule yule au mwanamke ni yule yule, mie naona itakuwa bora kama utamfundisha mwenzio nn unataka ili akupatie kuliko kutoka nje. maana sehemu zote za siri zinafanana kwa wanaume na wanawake.

No...sio kweli. Hujawahi kukutana na zilizopinda? zilizonyooka? nene? nyembamba? zilizokatwa? zenye maji? kavu? saa sita? vindimu? n.k.

Unachozungumzia wewe ni jinsia lakini watu ni tofauti. Kuna mambo mengi hapa...tangible na intangible ambayo unaweza kuyapata au kuyaona kwa fulani na usiyapate au usiyaone kwa mwingine. Sasa kwa mtaji huo utafanyaje maana kuna mambo mengine hayafundishiki....
 
Inabidi tu ulizike na ulichokipata. Nadhani utakizoea na kukipenda. Kutoka nje jamani maradhiiiiiiii!
 

Hatua ya kwanza ya kujibu swali lolote ni kulielewa swali lenyewe. Nimesoma majibu mengi humu yanayoonyesha wanaojibu wanatoa maelezo mengi na mazuri, lakini hawajibu swali.

Usemi kuwa "anayejuwa baba wa mtoto ni mama" una ukweli wenye uzito mkubwa sana. Lakini, ukweli huu si ukweli mtupu.

Ukweli unapatikana pale tu anapojuwa kwa uhakika kuwa aliyekwenda naye ndiye huyo huyo tu. Lakini ukweli huu unapungua thamani na uzito atakapokuwa amekwenda na watu zaidi ya mmoja.

DNA imekwisha waumbua akina mama wengi sana hata kama wanasema kwa nia nzuri au kwa kukosea kwa makusudi. Hali ambayo inathibitisha jibu langu.
 

Kuna kipindi kwenye TV ya Marekani ambacho single mothers huwaweka kiti moto wale wanaodhani kuwa ni Baba wa watoto zao ili wachangie malezi ya watoto. Hawa inaelekea kwa siku hutembea na mwanaume zaidi ya mmoja. Nasema hivi kwa sababu kuna mama mmoja aliwaita wanaume 10 na wote hawa walifanyiwa DNA kuangalia kama ni Baba wa mtoto ambaye mama alitaka mzazi mwenziye amsaidie pesa za matunzo na wote majibu yalionyesha kwamba hawakuwa wazazi wa mtoto yule. Kwa hiyo kama mwanamke ni mwingi mno si ajabu hata yeye asijue ni nani Baba wa kweli wa mtoto anayemdhania anaweza kabisa asiwe huyo.
 
 
Sababu ya kutoka nje ya ndoa ni tamaa ya fedha,ulimbukeni wa ngono na pepo ngono.Kwani hata wenye uwezo kifedha hutoka nje ya ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…