Je,Ni kweli kuwa matajiri Wengi hawa enjoy maisha?

Je,Ni kweli kuwa matajiri Wengi hawa enjoy maisha?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Niliwahi kusikia mahali kwamba heri masikini na watumwa wao ndo hawanaga stress kama boss eti kwamba matajiri wanateseka sana japo wana hela lakini haziwasaidii kupata furaha Wala kupata usingizi mzuri wala kuwa na amani ya moyo naombeni tu kujua kama ni kweli au ndo zetu maskini kujipaga matumaini.

Binafsi kwa uzoefu wangu me huwa na furaha hata nikiwa sina pesa ila pia nikipigika kisawasawa hata mzuka wa kupost JF nakuwa Sina thanks God naona labda kweli mwigulu kaweka trillion Tano kwenye system maana mazali yananitembelea now.
 
nina experience hali yangu tu matajiri siwezi kuwasemea kwasababu sijawahi ishi maisha yao
 
Acha utoto mkuu tajiri anakula bata chochote akitakacho anapata muda huo pisi kali grade one pombe classic gari kali account inasoma miamala hizo stress zinatoka wapi labda utajiri wa ndagu
 
Itategemeana na aina ya akili aliyenayo kichwani huyo tajiri maana mwingine atataka afatilie mpaka usafi wa chumba cha housegirl wake
 
Inategemea na utajiri huo umepatikana kwa njia gani, yupo tajiri mmoja, (jina kapuni) kila inapofika usiku yeye huchukua kigodoro kidogo na mto kisha huenda kulala sehemu za maporomoko au mabondeni na hudamka alfajiri sana...cha ajabu gari(basi za usafiri) zake zinafanya vema sana kanda ya kusini mwa Tanzania...Unaanzaje kufurahia maisha ktk hali hii?
 
ACHANA HIZO

STAREHE GHARAMA YAHEEEEE ,NA GHARAMA NI PESA.



Wewe bila Hela, utaenda Kwa Space huko kama alivyofanya Huyu Bilionea wa uingereza???.
 
Ukiwa na hela utaona hela si kila kitu, usipokuwa na hela utaona hela ndio kila kitu...
 
Utajiri uinakupa fahari ya maisha na sio peace of mind, watu wenye pesa nyingi ndo wanaongoza kwa stress.
Yaani wanachangnikiwa na maisha mpaka ukiona nyumba ndogo zao unabaki kujiuliza, huyu jamaa karogwa au vipi.....kwa nini anakuwa na demu kama hivi?
 
Inategemeana na njia iliyotumika kupata hizo pesa imagine umeiba au kudhulumu au hata kuua sasa hapo furaha utaitoa wapi????
Kuna wale wa masharti chungu nzima ndio kabisaaaa full stress
 
Back
Top Bottom