trachomatis
JF-Expert Member
- Jun 7, 2011
- 3,758
- 744
Wadau wa soka..Binafsi sidhani kocha yeyote anayejulikana kwa ubora ndiye muarobaini wa soka letu..Ukizingatia katika Afrika Mashariki sisi tuko nyuma kisoka(nafuu ilikuwepo wakati wa Maximo),sidhani kwa kigezo hicho tunaweza kuwa kama England ambao wanajiamini kwa ubora wa ligi na vipaji vya wachezaji wao. Kama kweli tuna nia ya kutafuta tunapokosea na upi muarobaini kwa soka letu labda iundwe TUME! Kama tume nyingine mfano ya rushwa ya Warioba.Mle ndani mna kila kitu,mianya mpaka ushauri wa jinsi ya kupambana nayo. Naamini sisi kama nchi hatujajua tatizo la soka letu.Tukijua hilo naamini uwekezaji wa makampuni ya vinywaji na taasisi kama mabenki utaenda mahali ambapo manufaa yake tutayaona with time. Karibuni wadau.