Suali zuri na ukweli huku hivi .
muhumu kujua kabla ya Islamic Republic kuanzishwa kujua Iran ilikua chini ya nani ? Iran ilikua chini ya Monacrch wa zaidi miaka 2000 chini ya Shah Mohamed reza Khan Pahlavi.
ufalme huu ulikua rafiki wa Israel , USA na South Africa ya Makaburu
Shah alikua kipenzi cha west na kibaraka mkubwa.Alitumika sana kuzorotesha uhuru wa baadhi ya nchi.
- Mfano miaka ya 70 kulikua na azimio la kuiwekea vikwazo Israel vya mafuta. Ncho zote za Opec zilikubaliana kuiwekea Israel vikwazo kutoka na ukaliaji wake wa maeneo ya Masri , Palestine, Syria na Lebanon, Vikwazo vile havikufanikiwa kwani IRAN chini ya Shah akitumiwa na West powers alivivunja na akawa ana supply mafuta Israel. Hivyo mpango ule uka fail.
- pili Wakati UN iliwekea vikwazo South Africa ikiwamo kuuzuwa Mafuta ili kuibana kuachana na siasa zake za kikaburu...jumuiya yote ya Opec na wazalishaji mafuta walikubaliana kuto kuuza mafuta Kwa makaburu.Ni IRAN tena chini ya Shah ikavunja mpango huo na ikawa inauza mafuta kwa makburu. ( Kuja kwa Ayatollah na Islamic Republic ilikatisha kuwapatia mafuta Mkaburu na ikawa ndio chachu ya kuanguka)
Khomein mwanzo alikua akiishi Iran na kutokana na upinzani wake kwa Shah akafukuzwa hivyo akaamua kuishi Iraq . Huko Iraq chini ya Sadam ambaye alikua darling wa West akalazimishwa kumfukuza na akaamua kuhamia France.
akiwa huko ndiko aliainzisha harakati kubwa za kumuondoa Shah kwa kutumia mwavuli wa imani ya wairan ya Kishia. akapa uungwaji mkubwa mkono na raiaa wengi ambao walichoka na mambo ya shah.
France hawakumzuia kufanya siasa akiwa huko, inawezekana France haikufaidika sana na Shah ambaye alielemea sana USA. hIVYO ILIACHIA Ayatollah anedeshe harakati zake nchini ufaransa.
akaitisha migomo na maandamano makubwa yasio na kikomo...askari wa Marekani na wale wa Shah walifanya kila mbinu za mateso na mauaji lakini raia hawa kusimama wala kuvunjika moyo.
Utawala wa shah ukaanza kuporomoka na Shah akakimbia siku Ayatollah alipotangaza anarudi IRan.
kitu interesting ni kuwa France walitoa ndege yao Airbus iliyo msafirisha Khomein kutoka France akiwa na familia yake na timu yake yote ya wapinzania iliokuwa ikiishi uhamishoni. Juhudi za USA, Israel na Iran na UK kuitaka France asimruhusu kurudi hazikusikilizwa na Ufarance ...hatimae Khomein alitua Teheran na Utawala kibaraka wa Shah Ukaanguka.
Hivyo utaona USA na other western countries hawakusaidia Kuanzishwa kwa Taifa la kiislam la Iran. Ufaransa alishiriki kusaidia moraly kwa tamaa ya kuwa na influence kwa utawala mpya. Ingawa hakufikiria kama utawala utakaongia utakua too extreme ...lakini upande mmoja France ndio bado wananufaiaka sana kibiashara na Iran mpya ingawa vikwazo vilizorotesha.
Hii video inaonesha siku za mwisho za Shah