Je, ni kweli maji ya AC yanafaa zaidi kuwekwa kwenye rejeta?

Je, ni kweli maji ya AC yanafaa zaidi kuwekwa kwenye rejeta?

zhang laoshi

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2014
Posts
434
Reaction score
581
Habari wadau,

Nimelipata sehemu hili kuwa maji yanayotoka kwenye AC za maofisin na majumbani ni bora zaidi na yanasaidia kupoza vizuri injini ya gari vizuri zaidi.

Wajuzi mnijuze.

Asante.

images%20(20).jpg
 
Kisa yanakuwa ni ya baridi?? 😀😀
Hizo ni sound (myth) kama sound zingine tu, manufacturer anasema tutumie recommended coolant... So kama huna mpunga wa hiyo special coolant tumia maji masafi yoyote tu...

Usije hangaika bure kutembelea ofisi za watu.
 
Kisa yanakuwa ni ya baridi?? [emoji3][emoji3]
Hizo ni sound (myth) kama sound zingine tu, manufacturer anasema tutumie recommended coolant... So kama huna mpunga wa hiyo special coolant tumia maji masafi yoyote tu...

Usije hangaika bure kutembelea ofisi za watu.
Hapana. Maji ya kwenye ac ni maji yanayopatikana baada ya hali ya mvuke kupozwa na kugeuka matone ya maji. Hayo maji huwa tunaita condensed water au distilled water.

Haya maji yanakuwa na sifa ya kutokuwa na impurities kama madini au chemical ambazo huwa ni corrosive kwenye maeneo ya ndani ya Radiator.

Pia maji ya mvua direct from the sky pia yanaweza kutumika ingawa hatari ya maji ya mvua miaka hii ni chemical gesi za hewani zinazotoka viwandani huwa zinayafanya hayo maji kuwa acidic.

Pia maji ya kunywa ya nyumbani yale ya kuchemshwa yanasifa hiyo ya usalama.

Maji ya battery ya baridi (sio yale ya moto au ya acid) nayo pia ni distilled water na unaweza tumia katika radiator.

Ila technology imekuwa na sasa tuna coolants so kiwango cha uhitaji wa maji kuweka katika Radiator ni kidogo au hakipo kabisa now days.
 
Back
Top Bottom