Je, ni kweli meli ya MV Ibn Khaldum ilileta silaha za Mapinduzi ya Zanzibari?

Je, ni kweli meli ya MV Ibn Khaldum ilileta silaha za Mapinduzi ya Zanzibari?

Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2020
Posts
5,200
Reaction score
12,762
Tarehe 2 Januari 1964, meli iliyofahamika kwa jina la Mv Ibn Khaldun ikiongzwa na kepteni Racchid Ben-Yelles ilitia nanga katika bandari ya Dar es Salaam ikitokea kaskazini mwa Afrika katika nchi ya Algeria ambapo ilikuwa imebeba shehena ya silaha kwa ajili ya kusaidia ukombozi katika nchi ya Msumbiji na kwa ajili ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Meli hii Mv Ibn Khaldun ilikaa katika bandari ya Dar es Salaam kwa siku nane tarehe 2 januari 1964 mpaka tarehe 9 januari 1964 na mara ilipo fika ilikaa mbali kidogo na bandari ya Dar es Salaam kwa masaa arobaini na nane. Aliyekuwa rais wa Tanganyika kwa wakati huo Mwl. Nyerere akiwa na bwana Djoudi ambaye alikuwa 'Charge d'Affair' katika ubalozi wa Algeria Tanganyika katika kuikagua meli hiyo.

Kwa amri ya aliyekuwa swahiba wa karibu na Mwl. Nyerere bwana Oscar Kambona aliamrisha silaha hizo zipakuliwe chini ya uongozi ya kepteni Nyerenda na kuwekwa katika ghala la Public Works Department (P.W.D) na alipohitajika na waandishi wa habari juu ya kutoa maelezo zaidi juu ya silaha hizo bwana Kambona alikwepa sana mahojiano na waandishi wa habari.

Kuna maswali kidogo muhimu ya kujiuliza juu ya ujio wa meli hii na kuonekana kushiriki kwa karibu kwa serikali mbili yaani serikali ya Tanganyika na serikali ya Algeria na viongozi wao.

[emoji117]Je, serikali ya Algeria na Tanganyika zilikuwa zinajua mpango wa mapinduzi ya Zanzibar?

[emoji117]Algeria ni nchi ya Kiarabu na serikali ya wakati huo ya Zanzibar ilidaiwa kuwa ya waarabu kivipi Mwarabu awe katika mpango wa kumpindua mwarabu mwenzake tena akishirikiana na serikali ya Tanganyika?

[emoji117]Mwl. Nyerere kwa namna moja au nyingine alikuwa 'master mind' wa kufanikisha mapinduzi ya Zanzibar kwa lengo baadaye kuja kuungana nayo? Maana hata uko tunaona Mwl. Nyerere aliwahi kuwatoa baadhi ya watu kwa Karume ambaye alitishia kuvunja muungano kama Nyerere angeendelea kuwalinda hao watu mfano wakina Kasimu hanga. Babu nk ili kulinda muungo hivyo Mwl.Nyerere hakuona shida kushiriki katika mapinduzi ili kutimiza dhamira yake ya Muungano au kuwatoa watu fulani ili kulinda muungamo.

[emoji117]Je, ilikuwa ni dhamira ya dhati ya Mwl. Nyerere kuunganisha nchi hizi mbili kwa kigezo cha historia, lugha na tamaduni pasipo msukumo kutoka nje?

Karibuni wajuzi wa historia kutupa darasa.
 
Hatutakiwi kulijadili jambo hili lililopitwa na wakati, Moderator, naomba uufungie uzi huu kama ulivyoufungia wa kwangu wa "KUTABIRI MAMBO YAJAYO" past and future are not here today.
Kujadili jambo lolote halija wahi kuwa kosa,maana malengo ya mijadala mbalimbali ni kujifunza.Hivyo sioni mantiki ya kufuta Uzi ikiwa lengo ni kutaka kujifunza mkuu.
 
Muulize mzee wetu Mohamad said anayetokota na kujaa upepo huko Azam TV Channel namba 108 Sasa kwenye kipindi cha "Baragumu" baada ya Azam kuweka Documentary inayomtaja Mkristo na Mganda Bwana John Okelll kuwa ndio Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar.😀😃😄😁😆😅
 
Muulize mzee wetu Mohamad said anayetokota na kujaa upepo huko Azam TV Channel namba 108 Sasa kwenye kipindi cha "Baragumu" baada ya Azam kuweka Documentary inayomtaja Mkristo na Mganda Bwana John Okelll kuwa ndio Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar.[emoji3][emoji2][emoji1][emoji16][emoji38][emoji28]
Mzee huwa na maarifa mazuri na bora kabisa,shida yake kubwa ni udini hivyo kufanya watu kupuuzia mambo yake mengi sana.

Kuhusu Bwana John Okello mbona iko wazi kwamba ndiye Shujaa wa mapinduzi ya Zanzibar.
 
Back
Top Bottom