Kwa kifupi kuna dawa ambazo zina muingiliano wa moja kwa moja na pombe na huweza kusababisha madhara makubwa hata kifo ukitumia pamoja na pombe, mfano wa hiyo dawa ni flagyl/metronidazole dawa ambayo wengi tumeshaitumia na tunaijua.
Kwa upande wa dawa ya Viagra haina uhusiano wa moja kwa moja na muingiliano na pombe, kwa muingiliano inamaanisha drug interaction.
Kutokuwepo kwa muingiliano wa moja kwa moja kati ya pombe na dawa isiwe sababu ya kigezo cha kutumia dawa na pombe, sababu matumizi ya pombe yanaweza yakasababisha matumizi yasiyo sahihi ya dawa( irrational use of drug), au kupelekea maamuzi yasiyo mazuri wakati unatumia dawa.
Ngoja nikupe historia fupi ya jinsi viagra ilivyogundulika hadi kupelekea matumizi yake mpaka sasa.
Zamani kulikuwa dawa iliyoitwa sildenafin citrate na ilikuwa inatibu na wanapewa wagonjwa/wateja wenye tatizo la shinikizo la juu la damu( high blood pressure), kilichotoke wale waliokuwa wanatumia hiyo dawa ambayo ndio ilikuja kujulikana kama Viagra ni kwamba walipata maudhi madogo ya mboo kudinda isivyo kawaida kwa wagonjwa/wateja wanaume.
Kwa hiyo wengi waliopewa dawa hii kutibu presha iliwasaidia kushuka presha ila pia mlingoti ulikuwa ukisimama isivyo kawaida, baadae wataalamu wakaona hayo maudhi madogo/side effect yanaweza yakawa na faida kwa wanaume wenye matatizo ya kudindisha( Erectile dysfunction syndrome). Ndivyo ilivyokuwa kwa kifupi.
Turudi kwenye mada ili mboo/mlingoti/mshedede/mkuyenge uweze kudinda ipasavyo inahitajika mishipa ya damu ipate kwa wingi mzunguko wa damu wa kutosha na ndio mashine inasimama dede, kinachofanya viagra ni kusaidia mzunguko wa damu sehemu zile za kichwa cha chini kuwa mkubwa na kupelekea mdude kusimama, athari inayoweza kutokea ni kuwa kwa kuwa viagra ina weza kushusha presha ikitumiwa na kiasi kikubwa cha pombe inaweza ikapelekea presha kushuka isivyo kawaida( low blood pressure) ambayo inaweza ikasababisha madhara hata kuhatarisha maisha hasa wenye matatizo ya presha.
Wajuzi wengine watajazia nyama