Je, ni kweli mwanamke mwenye kitambi hupoteza mvuto?

Tatizo sisi wanaume saa nyingine tunakuwa kama tumelaaniwa na aliyetulaani hataki kufuta radhi. Nini maana yake? Wewe mwaume una bonge la kitambi halafu sijui unatoa wapi ujasiri wa kumwambia rafiki yako wa kike kwamba ana tumbo kubwa na anachukiza. Sasa kama ndio hivyo wewe ulimpenda mtu au ulipenda ukubwa wa tumbooooo.....? Kwa wale ndugu zangu wenye akili fupi kama za ........ waache huo ujinga mara moja au hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao kwa kitendo cha kudhalilisha mama zetu kwamba wana tumbo kubwa. Na kingine kama sio hilo tumbo unalosema leo ni kubwa na linachukiza wewe ungekaa wapi? na je ungekuja duniani? FIKIRI KABLA YA KUONGEA. Saasawa kujana?
 
Ndio Kitambi cha mwanamke kinapoteza mvuto na hamu kabisa ya mapenzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…