Je, ni kweli Serikali haina Dini?

Je, ni kweli Serikali haina Dini?

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Huwa sielewi huu msemo kwamba serikali haina dini.

1. Kwenye Ufunguzi wa Vikao vya Bunge kuna dua ya kumuomba Mungu.

2. Kwenye Viapo vya Teuzi za Viongozi wa Serikali humuomba Mwenyezi Mungu awasaidie kutimiza viapo vyao.

3. Wimbo wa Taifa unamuomba Mungu kulibariki taifa.

Au kusema Serikali haina dini ni tofauti na kusema Serikali haiamini uwepo wa Mungu?!
 
Serikali haina dini, ila watu wake wana dini.. na haiwezekani tenganisha serikali na watu wake... 😵‍💫😵‍💫
 
Huwa sielewi huu msemo kwamba serikali haina dini.

1. Kwenye ufunguzi wa vikao vya bunge kuna dua ya kumuomba Mungu

2. Kwenye viapo vya teuzi za viongozi wa serikali humuomba Mwenyezi Mungu awasaidie kutimiza viapo vyao

3. Wimbo wa taifa unamuomba Mungu kulibariki taifa

Au kusema serikali haina dini ni tofauti na kusema serikali haiamini uwepo wa Mungu???!!
Wasikuchanganye kwakuwa serikali ni watu na hao watu wana dini zao
 
Huu ni mwaka 2023. Miaka zaidi ya 2000 tangu yesu afufuke na kupaa. Hivyo jibu unalo serikali ni wakristo.
 
Nafikiri uelewa ni tofauti hapa! Mi naelewa serikali Haina dini kwa maana hii watu wote itawahudumia bila tofauti ya dini zao ama tofauti zao ktk namna yoyote.

Pili serikali inamambo yake ambayo inasheria zake zinazoamuliwa kiserikali pasipo mitazamo ya kidini mfano mahakama zinavyoendesha kesi na hukumu, kwenye dini usiue lkn serikali ikikukamata na hatia ya mauwaji unalamba kamba!..

Fumbueni macho msichanganye vitu....
 
Inaamini kuwa kuna Mungu.
Huo ni utashi wa mtu na sio serikali yetu na imetoa uhuru wa kuabudu hivyo wao hata wakikuita uwaombee sioni kama ni tatizo maana ktk namna Moja au nyengine watu mmoja mmoja wanaimani zao tofauti na Kuna kitu kinaitwa taifa ambalo limeunga hizo Imani zote so wakiegemea upande fulani huko watachana bendera.
 
Huwa sielewi huu msemo kwamba serikali haina dini.

1. Kwenye Ufunguzi wa Vikao vya Bunge kuna dua ya kumuomba Mungu.

2. Kwenye Viapo vya Teuzi za Viongozi wa Serikali humuomba Mwenyezi Mungu awasaidie kutimiza viapo vyao.

3. Wimbo wa Taifa unamuomba Mungu kulibariki taifa.

Au kusema Serikali haina dini ni tofauti na kusema Serikali haiamini uwepo wa Mungu?!
Inaamini uwepo wa Mungu huwa kinachofanyika ni hawataki kuweka matabaka Kati ya nchi na wananchi wenyewe nafikiri umenielewa
 
Sijui huyo Mungu wanaye mtaja amewasadia nini hadi sasa ?

Hizi ni akili za kipumbavu kuendelea kumtaja taja huyo Mungu kwenye mambo ya serikali zetu
 
Back
Top Bottom