Je, ni kweli Serikali ya awamu ya tano imewajali masikini?

Je, ni kweli Serikali ya awamu ya tano imewajali masikini?

JET SALLI

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2014
Posts
2,392
Reaction score
1,578
Watu wengi sasa wameona na wametofautisha ni wakati gani kati ya awamu hii na ile iliyopita ya KIKWETE ni wakati gani umasikini umekolea vzr na majibu yako wazi na yanajulikana wala hayahitaji mtu apewe michoro ili aelewe vzr.

Serikali ya awamu ya tano ilijinasibu,na imeendelea kujinasibu kuwa ni serikali ya wanyonge,swali linauliza, hivi ni kweli hii ni serikali ya wanyonge na hapo ndipo utajua kwamba kuongea ni rahisi sana ili utekelezaji ni jambo gumu sana hasa kwa CCM hii tuliyonayo,hebu angalia magari anayoyatumia Rais Magufuli kwenye kampeni zake karibia gari nyingi ni V8 ambazo gharama zake zinakaribia milioni 400 kwa kila gari moja hiyo ndio serikali ya wanyonge na huyo ndio kiongozi wa wanyonge.Nimeamini sasa kwa nini YESU aliwaasa na Aliwahimiza wanafunzi wake wajitenge na UNAFIKI.

Tulipotoka awamu ya NNE tulikuwa tumeanza kwenda vzr wala hakukuwa na sababu ya kurudi nyuma,Leo baadhi ya watanzania wanashabikia serikali kununua Ndege sijui kama ni akili nijuavyo mm au ni UNAFIKI TU watu hawataki kusema ukweli hasa katika wakati huu wa ulimwengu wa utandawazi.Huwezi kung'ang'ania kununua ndege za watu wachache ukasahau huduma kwa mamilioni ya watu.

Unaposema unasimama na WANYONGE NA MASIKINI UNATAKIWA UWEKE UNAFIKI PEMBENI na kauli yako ikisema hiki ni kikombe na iwe hivyo na isiwe unamaanisha kwamba ni bakuli.

FUNZO hili liwe ni kwa vyama vyote na si kwa CCM pekee.ULEVI NI KITU HATARI sana mlevi sikuzote halei familia hata kidogo ss wote tunaelewa.ULEVI WA MADARAKA ni MBAYA ZAIDI kwa sababu unaweza kulitumbukiza Taifa ktk matatizo makubwa.Kutotenda HAKI NI KUBAYA ZAIDI KWA SABABU kunajaza hasira ktk mioyo ya watu na mlipuko wake nadhani hakuna BOMU linaloweza kufanana nao.

Nawashangaa sana VIONGOZI wa dini wanaozungumzia AMANI TU SIJUI KAMA WANAELEWA VZR.Nadhani wana uelewa finyu kwamba ETI amani IPO na haibebwi na kitu chochote.

TUKUMBUKE AMANI ni tunda la HAKI,Kwa maana ya kwamba MTI NI HAKI NA MATUNDA YAKE NI AMANI,JE UKIUKATA MTI UNAWEZAJE KUSUBIRI MATUNDA?WATANZANIA HAWAHITAJI VIONGOZI WASIOJUA WANAONGEA NN.
 
Walimu wastaafu Halmashauri ya kilombero wa tangu 2016 hadi wastaafu wa 2019 achilia mbali wa 2020 bado kupata nauli za kuwarudisha makwao. Chama cha walimu mtusaidie kuna shida gani. Tumeduaa hatujui la kufanya.
 
Imewasomesha namba zaidi, wengi walishasahau hata kunywa chai, watu Wana shindia mihogo, watoto wanaokota makopo ili wajihudumie sababu ya ugumu wa maisha wazazi wamesambaratika yote ni kwa sababu ya mtu mmoja anaesaza na kuvimbiwa Kodi zao
 
Walimu wastaafu Halmashauri ya kilombero wa tangu 2016 hadi wastaafu wa 2019 achilia mbali wa 2020 bado kupata nauli za kuwarudisha makwao. Chama cha walimu mtusaidie kuna shida gani. Tumeduaa hatujui la kufanya.
Mwalimu mwenzenu ajuaye shida zenu amewasahau
 
Sii kweli, imejali zaidi maslahi,yake iliyojipa Kama kipaumbele.
 
Mtetezi wa wanyonge anapowanyonga wanyonge, hii uleta Sana shaka.

Tangu nchii hii iumbwe hakuna awamu mtz anaishi maisha ya mbwa Kama awamu hii iliyowaletea watu ufukara kwa kuwasomesha namba ili wawe masikini kimakusudi ili waweze tawaliwa
 
Serikali haijajali kabisa masikini wala watu wa kipato cha kati. Wanaokula maisha ni makundi machache ambao mheshimiwa rais anaamini anawahitaji ili kuendelea kubaki madarakani salama.
 
Waliofaidika zaidi na utawala wa Magufuli ni mabeberu ndege za mabeberu zimenunuliwa kwa fedha tasilimu wakati nchi nyingine hawanunui kwa fedha tasilimu wanakopa na bado ndege hizohizo zinawabeba mabeberu kuwaleta nchini, miradi yote mikubwa inayojengwa na mabeberu wanalipwa tasilimu bila kukopwa wakati kwa mwananchi kulipwa tasilimu imekuwa ndoto kwake sanasana wananchi ndio wanakamuliwa hata kidogo walichonacho wanapewa mabeberu.
 
Awamu hii ni sawa na baba awanunuliae wanawe sabuufa, suti za milioni 4,tv za milioni 3 watoto wake wenye njaa, waliokosa ajira, waliofukuzwa ada, wagonjwa. Vipaumbele vya watawala badala ya vipaumbele vya wananchi
 
Serikali haijajali kabisa masikini wala watu wa kipato cha kati. Wanaokula maisha ni makundi machache ambao mheshimiwa rais anaamini anawahitaji ili kuendelea kubaki madarakani salama.
Wakurugenzi,wakuu wa vyombo, viongozi wa dini wachumia tumbo, wasiojulikana,watu wa propaganda kina musiba na bashite.
 
Watu wanatekwa, wanapigwa risasi mchana kweupe, wanauawa, na wanafilisiwa kwa maagizo toka kwa jiwe. Halafu anatokea mtu anasema anajali.

Labda kama maana ya neno "kujali" limmebadilika maana.
 
Leo tunaona kwenye kampeni Eti wagombea wa CCM wanapiga magoti kuomba kura kwa wananchi,haya ndio maigizo wanayofanyiwa wananchi wa Tanzania,Leo tumeona Stamico wametoa gawio kwa serikali swali la msingi haya magawio yana faida gani kubwa toka yameanza kugawiwa.Leo ktk Tanzania ni rahisi kwa mtu mwenye uelewa mdogo kuwalaumu baadhi ya watanzania kuwa wanakosa uzalendo kwa taifa lao huku akisahau kwamba MATUNDA au mema ya nchi yanaliwa na watu wachache na hawajali matatizo ya wananchi walio wengi, alafu MTU anataka watu waliosoma kwa mfumo wa hovyo wa Elimu ya Tanzania na kwa sasa anatumikia adhabu ya kukosa ajira awe mzalendo wa kweli kwa Taifa.Watawala wetu sio viongozi maana wangekuwa viongozi wangeonesha njia ili kunusuru Taifa letu na chuki inayoendelea kukua kila siku na kila kukicha dhidi ya serikali ya CCM kwa sababu vijana hawana ajira,wastaafu hawalipwi kwa wakati mafao yao,kodi na tozo mbalimbali ni kubwa,hali ngumu ya maisha,watu siku hizi hawastaafu wala kufa tena ndio maana hakuna ulazima wa kuajiri watumishi wapya ili kuziba nafasi.Yote haya serikali ya awamu ya tano inadhani watanzania wanafurahia,na ninaamini hakuna mtanzania awe mwana CCM ,CHADEMA ,CHAUMA,UDP,TLP,ACT ambae ndugu yake au mtoto wake hajaguswa na maumivu yaliyoletwa na serikali ya CCM ya awamu ya tano.wapo walioachishwa kazi na ninaamini kati yao ni wazazi wetu ss watanzania ambao ss watoto wao tunapatikana ktk kada mbalimbali za utumishi tena wengine walikuwa wanakaribia kustaafu hata huruma kidogo tu hakuna pamoja na utumishi wa miaka mingi wa wazee hawa,sasa nao hawa wakilalamika tutasema sio wazalendo.Serikali inapaswa kuwa na huruma kwa watu wake na si kuwatenda JEURI kama ilivyofanyika vyote hivi vinajenga hasira kwa watanzania matokeo yake tunaanza kuzurura na wasanii ili kuvutia watu kwenye mikutano kwa sababu tunajua tusipo Fanya hivyo hakuna MTU atakae kuja kwa sababu tunajua tumevurunda pakubwa.Ni wakati wa kuvuna tulichopanda ukilima mahindi huwezi kuvuna maharage.Ukilewa pombe vzr lazima upotee njia.
 
Back
Top Bottom