Je ni kweli Simba sasa ina wapenzi wengi kuliko Yanga

Wapo wengi sema wameinamisha vichwa maana kwa sasa kila kona ni kipigo cha mbwa koko, subiri wakianza kushinda, sijui lini!!
 
Tuma salamu kwa watu watatu
 
Hizo ni porojo za Haji Manara kwamba Simba ina mashabiki wengi zaidi.

Hakuna anayejua kila timu ina wanachama na mashabiki wangapi. Hakuna. Kila kitu ni perceptions na unazi wa timu.

Wakati Yanga ikiwa inafanya vizuri, mashabiki walikuwa wengi Uwanja wa Taifa kuliko wale wa Simba. Sasa ni kinyume. Wengi wanakuwa wa Simba. Ni uzwazwa ku conclude kwa kutumia kigezo hicho.

Kati ya Yanga na Simba, timu ipi inajua idadi ya wanachama wake? Jibu ni hakuna. Hadi uchaguzi, ndiyo hutokea hamasa ya kulipia kadi kupata haki ya kupiga kura. Wakati mwingi hulipiwa na wagombea!

Timu ipi ina taarifa rasmi za mauzoya jezi? Hakuna!

Wingi wa mashabiki huendana na performance ya timu.
 
simba ina washangiliaji tu siku wakifunga ndo wanaonekana
 
Ukizaliwa Tanzania ukafahahamu kwamba kuna kitu kinaitwa mpira, automatically wewe ni Simba au Yanga. Kwa Tanzania sasa hivi simba ina fans wengi, hata ukisample kwenye group la watu, utakuta wengi ni Simba
Hizo sampuli zako zinakudanganya! Ya nini tuandikie mate na wino upo? Mods hebu tutengenezeeni thread ya kupiga kura hapa tuoni ipi ina mashabiki wengi hata hapa jf tu!!
 
Ni kweli Simba imefanya vizuri sana msimu huu kuanzia utawala mpaka benchi la ufundi na hata uwanjani kazi yao ni nzuri na inaonekana dhahiri, Lakini Yanga ina wapenzi & mashabiki wengi kuliko Simba, Mashabiki wa Yanga wamechoshwa na mwenendo mbovu wa klabu yao sambamba na kuyumba kifedha (kiuchumi). Wamekata tamaa na matokeo wanayoyapata klabu yao, Ziko sababu lukuki zinawafanya mashabiki wa Yanga wasiingie uwanjani. HONGERA WATANI WANGU SIMBA, MKO VIZURI SANA MSIMU HUU!
 
Yanga ina mashabiki wengi kuliko Simba.
Hii inatokana na historia yake.
Kuwa
Yanga ilianzishwa zamani zaidi kuliko Simba.
Yanga ilikuwa na mahusiano na siasa za mwanzo za TZ.
Yanga ilikuwa ni moja ya matawi kazi ya chama tawala kuanzia TANU hadi CCM.
Viongozi wengi wa zamani wa Chama na Serikali ni wapenzi wa Yanga hadi hii leo jambo lililo enda hadi kwa familia zao.
Yanga hapo awali ilikuwa kama timu ya wananchi wa TZ.

Simba ina washabiki wa wastani ambao wanauwezo kwenda uwanjani kama timu yao inafanya vizuri,
Washabiki wa Simba wana uwezo wa kipesa kuliko wale wa Yanga hivyo timu ikiwa inashinda wanaweza kuujaza uwanja wa Taifa na wengine wakabaki nje kwa kutotosha. [emoji1]
Yanga hata wakiwa wanashinda washabiki wao hawaingii wengi sana uwanjani sababu ya hali yao kuwa ngumu kimapato, wengi wanaoenda uwanjani huishia nje ya uwanja hadi mwisho wa mchezo ndio maana hatuwaoni wakiujaza uwanja hata kama timu yao inashinda kila mechi [emoji5]
Therefore to Conclude, Yanga inawashabiki wengi ila wachache ndio wenye uwezo wa kuingia uwanjani.
But Simba inawashabiki wa wastani wenye uwezo wa kuingia uwanjani kwa wingi kupita wale wa Yanga. [emoji1]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…