SoC01 Je, ni kweli tatizo la Ajira kwa Wanazuoni Wahitimu huchangia kudorora kwa uchumi nchini Tanzania?

SoC01 Je, ni kweli tatizo la Ajira kwa Wanazuoni Wahitimu huchangia kudorora kwa uchumi nchini Tanzania?

Stories of Change - 2021 Competition

Atosha01

New Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
1
Reaction score
0
Utangulizi

Kwa mtazamo chanya wa swali hilo tunaweza kujibu ni kweli, lakini tukiangazia mtazamo hasi tunaweza kutumia tatizo hilo kama fursa ya maendeleo ya kiuchumi. Je tunawezaje na kwa njia zipi? Basi Makala hii itaelezea mtazamo hasi kwa serikali na raia wake katika kupunguza tatizo la ajira nchini.

Wanazuoni Wahitimu ni akina nani?

Wanazuoni ni wanafunzi wa ngazi mbalimbali (yaani ngazi ya astashahada, stashahada, na shahada) waliojikita katika kusomea taaluma mbalimbali kwa ngazi tofauti ambazo wanamatarajio nazo kuwa kama ajira kwao kwa baadae (yaani baada ya kuhitimu mafunzo hayo). Wanafunzi hawa wakimaliza masomo yao na kufaulu kulingana na matakwa ya chuo husika hutunikiwa cheti na kuwa Wanazuoni Wahitimu wa taaluma fulani kulingana na taaluma walizosomea.

Ajira ni nini?

Ajira ni nafasi ya mtu katika kuajiriwa na mtu mwingine, ama taasisi ama kampuni kwa lengo la kutimiza majukumu au kufanya kazi kwa makubaliano ya kupata ujira kutokana na kazi hiyo

Aina za Ajira

Kuna aina mbili za ajira ambazo ni:
  • Kujiajiri na
  • Kuajiriwa
Kujiajiri
Ajira ni pale ambapo mtu mwenye mtaji wake binafsi anautumia katika kuwekeza katika biashara, ama kufungua kampuni kwa lengo la kupata kipato chake binafsi. aina hii ya ajira na

Makala

Je ni kweli tatizo la Ajira kwa Wanazuoni Wahitimu huchangia kudorora kwa uchumi nchini Tanzania?

Kuajiriwa

Ajira ni mtu anaajiriwa kwa maandishi/mkataba na sekta binafsi/sekta ya umma kwa makubaliano ya kufanya kazi fulani na kulipwa ujira kulinaga na masharti/vigezo vilivyopo katika mkataba. Kutokana ukosefu wa mitaji na pia ukweli kwamba wanazuoni wahitimu ni wengi kuliko nafasi za ajira hivyo kupelekea ajira kuwa tatizo nchini.
Na hapa ndipo kiini cha Makala hii. Mimi na wewe tujiulize kwamba tatizo hili linaweza kuchangia kudorora/kupungua kwa ukuaji wa uchumi nchini.

Mtazamo Chanya

Tukiangazia mtazamo chanya tunaweza jibu ndio kwa kuzingatia vyanzo vya mapato ya serikali huwa ni:
  • Mapato yatokanayo na Kodi
  • Na mapato yasiyotokana na kodi
Kwa asilimia kubwa Mapato yatokanayo na Kodi ndio chanzo kikubwa na cha kwanza kutegemewa katika kuchangia ukuaji wa maendeleo ya nchi kiuchumi. Yaani mapato hukusanywa na kutumika katika matumizi ya maendeleo ambayo huchochea kwa asilimia kubwa ukuaji wa uchumi.
Hivyo tunaweza kusema ni kweli tatizo la ajira linaweza kuchangia kodorora kwa ukuaji wa uchumi nchini kwa sababu zifuatazo:
  • Inapunguza kodi ya mwajiriwa (PAYE).
  • Inapunguza uwezo wa manunuzi (Purshasing power) ambapo zingeweza kuongeza kodi kama kodi ya ongezeko la thamani (VAT).
  • Inasababisha wimbi kubwa la vijana wa mtaani (yaani vijana wa vilingeni wapiga stori tu wasiofanya kazi)
  • Inachelewesha maendeleo kutokana na serikali kutumia nguvu nyingi katika kuelimisha na kuhamasisha vijana kutafuta njia mbadala kwani ajira ni tatizo.
Mtazamo Hasi

Niwazi kuwa kuajiriwa kumekuwa tatizo ni tatizo kubwa nchini. Swali je kujiajiari pia nalo ni tatizo? Hapa majibu yanakuwa na ukakasi kulingana na kila mtu sababu zake na mtazamo wake katika kujiajiri.
Lakini changamoto kubwa kwa waliowengi katika kujiajiri ni Ukosefu wa Mtaji wa kujiajiri.
Mtaji wa kujiajiri ni nini?


Mtaji ni kitu au rasilimali ambayo mtu anaweza kuitumia ili kuanzisha biashara. Rasilimali hii ndio ambayo itamfanya mtu yeyote aweze kuanzisha biashara ama kujiajiri.

Aina za Mitaji ya kujiajiri

Aina za mitaji tunaweza kuzigawa katika makundi matatu:
  • Mtaji uhai
  • Mtaji wazo
  • Mtaji pesa
Mtaji Uhai

Huu ni mtaji muhimu sana kwani huwezi kufanya jambo lolote ukiwa maiti ama umefariki ukiwa hai ndiyo uaweza ukafanya vitu vikatokea, hivyo hunabudi kujikita katika kuthamini uhai wako kwa kuutumia ipasavyo ili uweze kufanikiwa.

Mtaji Wazo.

Mtaji huu nao ni muhimu pia kwa mtu anayetaka kujiajiri kwani hapa ndipo akili na uwezo wa kufikiri hutumika katika kuamua nini natakakufanya ili niweze kupata kipato cha kwangu mwenyewe. Ipo haja kwa mtu anayetaka kujiajiri kujiuliza maswali yafuatayo ili kuwa na mtaji wazo wenye tija:
  • Mimi ni nani?
  • Nataka kuwa nani?
  • Nifanyeje niwe navyotaka kuwa?
  • Wakina nani watanisaidia nifike napotakafika?
Mimi ni nani? swali hili husaidia kujitambua kwa mtu na kuweza kwenda na muda ili asiweze jutia baadae kama alipoteza muda.
Nataka kuwa nani? humsaidia mtu kuweka malengo mzuri na thabiti kufika pale anapotakafika.
Nifanye nifike napotakafika? humsaidia kuweka mikakati/njia/hatua za kufanya ili kutimiza malengo.
Wakina nani watanisaidia nifike napotakafika? litamsaidia kuchagua watu sahihi watako msaidia/kumuongoza katika mapambao yake hadi kutimiza malengo yake.

Mtaji Pesa

Huu ndio mtaji wa mwisho kabisa baada ya kuwa na mitaji hiyo miwili ni rahisi sana kufanikiwa kwenye biashara kaama ukiwa na uhai na wazo hata kama hauna mtaji pesa kwa sababu utakapopata Mtaji pesa basi itakuwa rahisi kutekeleza wazo lako kwa uangalifu zaidi.

Njia za kupata Mtaji pesa

Zipo njia kuu mbili za kuwa na Mtaji pesa ambazo ni:-
  • Mtaji binafsi
  • Mkopo
Mtaji binafsi

Huu ndio mtaji wa kwanza na rahisi kwa anayetaka kujiajiri kwani ni jumla ya pesa zake binafsi ndizo hutumika katika kuanzisha biashara ambapo kiuharisia wahitimu wengi hulalamika kutokuwa na mitaji binafsi.

Mkopo

Hii ni aina ya mtaji ambapo mtu anayetaka kujiajiri anaweza kuchukua pesa kwa mtu, taasisi za kifedha ama serikali kwa dhumuni fulani kwa makubaliano ya kurejesa pesa hiyo kwa riba ama bila riba.
Kwa kawaida kuchua mkopo kwa mtu ama kwenye taasisi za kifedha kama benki huwa kuna changamoto nyingi ambazo zinaweza kuwakatisha watu tamaa ya kuchukua mkopo.

Mchango wa Serikali

Wananchi wengi wamekuwa wakilalamikia serikali pasipo tambua jitihada zinayofanywa na serikali kwa ajili ya kutatua tatizo la ajira kwa raia wake. Je unafaha kwamba kila mwaka serikali hutenga kiasi cha pesa kwa ajili ya kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa vikundi vya vijana? Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021 serikali ilitenga jumla ya shilingi bilioni 1 kwa ajili hiyo.

Wananchi wananufaika vipi na pesa hizo?

Mara nyingi wananchi wengi hawanufaiki na pesa huu kutokana na kwamba vigezo vyake huwagusa hasa wale walioko katika kikundi Fulani kilichosajiliwa na kina malengo fulani.

Nini kifanyike ili pesa hizo ziweze kuongeza Ajira kwa mtu mmoja mmoja na sio vikundi vya vijana.
Maoni kwa Serikali


Ili fedha hizi ziwe na tija kwa raia mmoja mmoja nafikiri serikali ingebadilisha mfumo wa utoaji wa fedha hizo yaani zitolewe kwa mfumo wa mradi wa serikali kwa vijana waliokosa ajira. Ambapo serikali ingeweza kubuni Mradi/Miradi ambayo itachochea ajira na kuongeza kipato kwa serikali.

Kwa mfano embu tuangazie ajira ya udereva wa abiria wa gari ndogo kwa njia ya mtandao yaani (Bolt, taxfiy na uber).

Mfano billion 1 iliyotengwa kwenye bajeti mwaka 2020/2021 inauwezo wa kununua gari ndogo aina ya Toyota IST 100 ambazo tukizigawa kwa wilaya zilizopo mkoa wa Dar es Salaam kila wilaya itapata gari 20. Tafisi yake serikali itakuwa na uwezo wa kuajili vijana 20 kutoka kila wilaya kufanya kazi ya udereva wa gari hizo.

Muundo wa Ajira

Ajira hizo zitakuwa chini ya usimamizi wa kila wilaya ambazo zitatangaza ajira kwa vijana kwa ajili ya kufanya kazi ya udereva kwa mkataba yaani mwajiriwa ataendesha gari kwa muda wa miaka miwili, na baada ya kumaliza mkataba huo gari itahamishwa umiliki wake kutoka kwa umiliki wa serikali na kwenda kwa mwajiriwa (yaani gari itakuwa ya mwajiriwa rasmi)

Mfumo wa malipo

Waajiriwa wote wanaweza kutengenezewa akaunti kwenye mfumo wa malipo ya serikali kwa njia ya mtandao (GEPG), ambao hutatumika kupeleka mahesabu ya gari kwa kila dereva kwa kiasi kitakachokubaliwa kwa siku, wiki au mwezi wiki au mwezi kama itakavyoainishwa katika mkataba wa ajira.

Mapato kwa Serikali

Tungaze tasmini fupi ya mapato ya Mradi huu kwa serikali kwa kuchukulia hesabu ya dereva kwa mwajiri ni shilingi za kitanzania laki na themanini (TZS 180,000/=) kwa wiki.
Kwa dereva 1 kwa wiki atapaswa kurejesha kwenye akaunti yake TZS 180,000/= ambayo ni sawa na 9,360,000/= kwa miaka miwili sawa na TZS 18,720,000/= ambapo kwa mradi wote madereva 100 kwa wiki sawa TZS 18,000,000/= na TZS 936,000,000/= kwa mwaka sawa na TZS 1,872,000,000/= kwa miaka miwili.

Kwa Mwaka 1

Hivyo serikali ingeweza kutumia bilioni moja yote kwa manunuzi ya gari ndogo 100 sawa na asilimia 100 ya matumizi na kwa mwaka wa kwanza wanauweza kukusanya kiasi cha TZS 936,000,000/= sawa na asilimia 93.6 ya makusanyi na kubakiza kiasi cha asilima 6.4 sawa na TZS 64,000,0000/= kwa mwaka wa kwanza kama ilivyoainishwa katika jedwali la kwanza la makusanyo ya mapato kwa madereva kwa miaka miwili.

Kwa Mwaka 2

Mwaka unaofuata mwaka wa mwisho wa mradi serikali inauwezo wa kukusanya TZS 936,000,000/= sawa na asilimia 93.6 ya makusanyo na makusanyo kuzidi kwa asilimia 87.2 sawa na TZS 872,000,000/= kama faida itakayotengezwa na serikali kutokana na mradi huo kama ilivyoainishwa katika jedwali la pili la mrejesho wa mapato na matumizi:

Faida za Mradi
  • Serikali kuongeza ajira kwa vijana
  • Serikali kupata mapato.
  • Kupunguza wimbi la vijana wa mtaani.
  • Serikali kutengeneza ajira binafsi baada ya mkataba kuisha

Hitimisho
Kutokana na idadi kubwa ya Wanazuoni waliohitimu taaluma mbalimbali kuwa kubwa kuliko idadi ya Ajira ushauri kwao ni kama ifuatavyo:
  • Kutochezea fursa.
  • Kutoa mawazo yenye tija yanayochochea maendeleo kwa jamii na serikali
  • Kubuni mbinu mbalimbali ya kujikomboa kiuchumi.
  • Kuwa na watu sahihi hata kama ni wachache lakini wawe na msaada mkubwa kwako.


Makala hii imeandaliwa na:
Fraterne Martine Assenga
Jumla ya Maneno: 1500
Barua pepe:
cpassenga@gmail.com
Simu: 0786 969 432
Lengo:Kushiriki shindano la Andika, Ushinde la Jamii forum​
 
Upvote 1
Back
Top Bottom