kafuta ambele
Senior Member
- Aug 7, 2017
- 184
- 515
Wadada wa kazi wamekuwa ni kundi muhimu sana kwenye jamii lakini lazima tukubaliane kwamba kuna watu hali yao ya maisha haijafikia hatua ya kuweza kumuajiri mtu na kumlipa kama inavyostahili na kwa wakati. Lakini wamekuwa wakiajiri wadada wa kazi kama fashion tu.
siku hizi mtu anawasiliana na bibi wa mtoto inatumwa pesa kijijini huko ambayo nyingine inatumika kama nauli na nyingine anabaki nayo bibi yake. Mtoto ambaye kutokana na changamoto za hapa na pale ameshindwa kuendelea na masomo basi anakuwa hana chaguo.
wadada wa kazi wengi kutokana na umri wao kuwa mdogo wamekuwa hawapewi wao pesa yao bali anatumiwa bibi au mzazi kijijini lakini wengine huadiwa na maboss wao kwamba watalipwa wakiwa wanaondoka lkn mwisho wa siku wanazushiwa jambo kama wizi na tabia mbaya na kufukuzwa bila kulipwa bali kupakiwa kwenye bus na kurudishwa kijijini.
Kwa upande wa mishahara imekuwa ikianzia shilingi elfu hamsini na kuendelea ambayo kwa maisha ya sasa ni pesa ndogo ukilinganisha na mahitaji. Je ni kweli mshahara wa shilingi 50000 unaweza kumkomboa binti huyu kujikwamua kiuchumi na kufikia ndoto zake nyingine. Nafikiri ni vema serikali ingependekeza mshahara wa kiwango cha chini wenye tija ili kumfanya huyu baada ya muda fulani aweze kupata hata mtaji wa kuanza biashara yake.
Baadhi ya watu wamekuwa na moyo wa kipekee kwani huwapeleka wadada wa kazi kujifunza stadi za ushonaji cherehani na nyinginezo katika muda wao wa ziada na wanapojua kushona pesa yao ya mishahara wanawanunulia cherehani na kuwaruhusu wakajitegemee watafute pesa na kusaidia wazazi na wadogo zao waliowaacha vijijini. Hili ni wazo moja la kuweza kuwasaidia mabinti hawa yako mengine mengi pia.
Wadada wa kazi za majumbani pia wapo ambao si waaminifu na wamekuwa wakibadilika wanapofika mjini na kuanza tabia mbaya na kutofanya kazi vizuri mwishowe wanaangukia kwenye tabia za ukahaba na kuharibikiwa kabisa kimaisha.
Wito wangu ni kuwasaidia wale mabinti wanaojitoa kwa hali na mali kututunzia familia zetu tuwapo kwenye majukumu yetu kwa kuwalipa vizuri,kutowabagua na kuwaelimisha kama watoto wetu tu.
Mwisho wa yote kama unaona huwezi kumlipa binti wa kazi basi usimuajiri unadhulumu mtoto ambae pengine amejikuta anafanya hizo kazi baada ya kupoteza wazazi wake sio jambo zuri.
Tusameheane kwenye makosa ya uandishi na turekebishane pale ambapo nimeteleza wana jukwaa.