Je, ni kweli unaweza kuwa Genius ila ukawa ni Failure Academically?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Inasemekana ni rahisi mno kwa Genius kufanya Vibaya Kitaaluma (akiwa Shuleni na Chuo Kikuu), ila ni Vigumu kwa Mtu wa Kawaida (Slow Learner) anayefaulu sana Kitaaluma kuwa Genius kabisa.

Najiandaa sasa Kusoma tu 'Nondo' zenu Kali 'Great Thinkers' wa JamiiForums ambao nawakubali kuliko Maelezo.
 
ni kweli mkuu" Ngoja tusubiri nondo na references
Kwahiyo kumbe unaweza ukawa Unafeli sana Shuleni huku Chuo Kikuu ukiwa ni Mbobezi ( Mtukuka ) wa kupata 'Sups' za Kutosha tu lakini bado ukawa ni Genius?
 
Disclaimer: Hakujawahi kua na haitatokea genius SAUT, ogopa matapeli

Tukirudi kwenye mada, Genius wachache hupoteza appetite mapema na kutamani kumaliza/kugraduate ndani ya muda mchache tuu wa masomo

Kudharau masomo huwafanya kuanza vitu vingine nje ya shule na ku-concentrate huko na hii hupelekea wengi tuu kutomaliza na kurukia vitu vingine vitakavyoifanya akili yao ifanye kazi angalau kwa kiwango kikubwa.

Hupenda pia kuwa maeneo ambayo watapata ushindani angalau (darasa lenye watu smart), na hii inaondoa uwezekano wa genius yeyote ku-exist kwenye vyuo vya vilaza laza ikiwemo SAUT.
 
Kuna magenius wengi huku mtaa tunakula nao ugali wa donee na mchicha mtaani, ila kuna back bencher wengine wako mbali kimaisha
 
Kwanini unapenda Kukoleza ( Bold ) Maelezo yako / Maoni yako? au unataka kujiweka tofauti ili utambulike Kiurahisi na pia uonekane kuwa ni Mchangiaji mwenye Madini?
 
Inaonekana Genta aliambaaambaa na credit mpaka akibukia BUSISI UNIVERSITY
 
Inasemekana ni rahisi mno kwa Genius kufanya Vibaya Kitaaluma (akiwa Shuleni na Chuo Kikuu), ila ni Vigumu kwa Mtu wa Kawaida (Slow Learner) anayefaulu sana Kitaaluma kuwa Genius kabisa.

Najiandaa sasa Kusoma tu 'Nondo' zenu Kali 'Great Thinkers' wa JamiiForums ambao nawakubali kuliko Maelezo.
Genius huwa wanaona na kutenda nje ya upeo wa watu wanaomzunga na wanaweza wasimwelewe kabisa hadi kumdisqualify kama issue ya galileo na catholic kuhusu dunia ni mvilingo. Dunia ina magenius ambao mfumo umeshindwa kuwacommodate na kuishia kuwa vichaa na masikini wa kutupwa wakati wana maona ya kubadilisha dunia. Ni kweli tunaongozwa na akili ndogo zilizopata fursa na hawako tayari at any cost
 
Fact
 
Back
Top Bottom