Wakuu kuna ukweli wowote kwamba vichaa hawapati kipindupindu ukilinganisha vyakula wanavyo kula so salama kiafya reference mjadala wa wasanii wetu wa bongo...
Kuna kitu kinaitwa ku adopt.
Unapokuwa exposed katika mazingira fulan kwa muda , mwili unajenga hali au namna ya kujikinga na changamoto.
Mfano unapo pata nakozi au sugu mikononi baada ya kufanya kazi ngumu.
Lakini masuala ya afya hili la kinga lipo sana, na hii hutegemeana sana na uimara wa kinga na afya mtu kiujumla.
Chizi aanzi gafla tu kuanza kula vyakula vya ovyo kwa 100% inakuwa kidogo kidogo na nguvu hujengeka kidogo kidgo hadi pale anapokuwa anakomaaa. Lakini si kwa watu wote huweza kujenga hiii kitu, katika stage ya mwanzo ya kushambuliwa na wadudu husika wengine wanafail kutengeneza kinga kisha huugua na kufa.
Sio machizi wote wasioumwa wapo wanaumwa sana tu, ila watamwambia nani?? Wataenda hospital?? HAPANA hapa ndio maana huwakuti au kujua kuwa wanaumwa.
Lakini jingine, kuna kitu kipo kisaikolijia kwenye akili. Ukisema LAW OF ATRACTION....
KUWA KILE KILICHO JENGEKA AKILINI MWAKO KINA ASILIMIA KUBWA KUTOKEA, Wagonjwa wa akili wengi na hata watu wengine wanaotumia vema hizi sheria na kuziisha hupata matokeo husika.
Wazee wetu walikuwa na msemo mmoja....
"AWAZALO MJINGA NDILO LITALO MTOKEA...."