Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,915
- 3,422
Habari njema Matajiri Wawekezaji,
Karibuni kwenye mfululizo wa masomo yetu ya programu ya NGUVU YA BUKU, ambapo tunajifunza na kufanya uwekezaji kwa hatua ndogo ndogo na kujenga utajiri kwa uhakika.
Kauli mbiu yetu kwenye NGUVU YA BUKU, ambayo pia ndiyo imani yetu ni KILA MTU ANAWEZA KUWA TAJIRI. Hilo tuna uhakika nalo kwa sababu kwa fedha ndogo ndogo ambazo kila mtu anazipata, tukiziwekeza kwa muda mrefu kwa msimamo bila kuacha, tunaweza kujenga utajiri mkubwa.
Kwenye programu yetu ya NGUVU YA BUKU, kwa sasa tunafanyia kazi lengo la kuwekeza kidogo kidogo, kwa miaka 10 bila kuacha wala kutoa. Miaka kumi ni kipindi kizuri kwetu kujisukuma kufanya uwekezaji na kuweza kuona matokeo mazuri kutokana na muda ambao uwekezaji huo unakuwa umeongezeka thamani.
Swali ambalo baadhi tunajiuliza ni nini kitakachoendelea baada ya miaka hii kumi ya uwekezaji kuisha? Japo miaka 10 bado hata hatujaikaribia, ni vizuri kujua ni wapi hasa tunapoelekea na huu uwekezaji ili tusipotezwe na mambo yasiyokuwa na tija. Au kushawishika vibaya na kuharibu uwekezaji ambao tumeujenga kwa muda mrefu.
Kwa kuanza, miaka kumi ambayo tumejipa ya kufanya huu uwekezaji ni kuwa na namba ambayo tunaweza kuiangalia, kuifanyia kazi na kupata matokeo ambayo ni mazuri. Lakini nyuma ya lengo hilo ni kuijenga tabia ya uwekezaji kuwa sehemu ya maisha yetu, ili kwa kila kipato tunachoingiza tuweze kufanya uwekezaji.
Kitu cha kwanza tunachotaka kufikia kwenye uwekezaji tunaoufanya ni uhuru wa kifedha. Uhuru wa kifedha ni pale tunapoweza kuingiza kipato cha kuyaendesha maisha yetu bila ya kufanya kazi moja kwa moja. Yaani tunakuwa tumefanya uwekezaji ambao unazalisha riba inayotosha kuendesha maisha yetu.
Tumeshajifunza kukokotoa kiasi cha uwekezaji wa kuwa nao ili kufikia uhuru wa kifedha. Ambapo unachukua gharama za maisha kwa mwezi utakazokuwa nazo wakati huo na kuzidisha mara 100. Hiyo ni kwa sababu wastani wa riba unayopata kwenye uwekezaji ni asilimia 1. Hivyo kama matumizi yako yatakuwa ni sawa na riba unayopata kwenye uwekezaji, umefikia uhuru wa kifedha.
Kufanya kufikia uhuru wa kifedha kuwa lengo letu la kwanza ni kutupa uhuru wa kufanyia kazi ndoto nyingine kubwa tulizonazo. Unapokuwa na uhuru wa kifedha unaweza kufanya makubwa kwa kuchukua hatari ambazo wengine hawawezi kuzichukua.
Ni vigumu sana kufanya makubwa kwenye maisha yako kama huna uhakika wa kupata pesa ya kuendesha maisha yako ya kila siku. Hivyo kuwa na uwekezaji ambao unakupatia pesa hiyo kutakupa utulivu wa kupambania makubwa.
SOMA; Tahadhari; Usikope Fedha Kwa Ajili Ya Kwenda Kufanya Uwekezaji.
Kitu cha pili unachotaka kufikia kwa kutumia uwekezaji ni kujenga dhamana ambayo utaweza kuitumia kupata fedha za kufanya makubwa zaidi. Kwa wengi, kiasi cha uwekezaji wa kuwa na uhuru wa kifedha ni kidogo, lakini unataka kufanya makubwa. Hilo litakulazimu uwe na uwekezaji mkubwa zaidi ili uweze kupata mikopo mikubwa zaidi.
Dhamana ya uwekezaji, hasa kwenye masoko ya mitaji huwa inapendwa zaidi na wawekezaji kwa sababu ya urahisi wake kupata fedha pale mtu anaposhindwa kurejesha mkopo. Hivyo kujenga uwekezaji mkubwa ambao utautumia kama dhamana ni lengo la kufanyia kazi.
Kwa sababu hizo kubwa, uwekezaji unakuwa hauna mwisho. Uwekezaji ni kitu ambacho tutakifanya kwa uendelevu kipindi chote cha maisha yetu. Hivyo baada ya kumaliza miaka 10 ambayo tumejipa kwenye lengo la sasa, tutaendelea kufanya uwekezaji, tena kwa ukubwa zaidi.
Kadhalika hata baada ya kufikia uhuru wa kifedha, siyo mwisho wa kuwekeza, badala yake ndiyo uwekezaji mkubwa zaidi unapaswa kufanyika.
Hata pale unapofika hali ya kuamua kustaafu, yaani hufanyi tena kazi ya moja kwa moja na unategemea uwekezaji wako kuendesha maisha, bado unapaswa kuendelea kuwekeza. Riba unayopata kutoka kwenye uwekezaji wako unapaswa kuendelea kuiwekeza.
Moja ya vitu unavyopaswa kuzingatia ni kuhakikisha uwekezaji wako hauishi ukiwa hai. Yaani hata ikitokea huwezi tena kuingiza kipato, uwekezaji ulionao usiumalize ukiwa hai. Unapaswa kuhakikisha mpaka unafariki dunia, hujamaliza kutumia uwekezaji wako.
Kwa kuwa na uhakika wa kipato kutokana na uwekezaji kunafanya maisha kuwa bora. Ukimaliza uwekezaji wako ukiwa bado hai, ubora wa maisha unashuka na kifo kinakuwa cha haraka zaidi.
SIKILIZA SOMO HILI KWENYE ONGEA NA KOCHA.
Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA tumekuwa na mjadala mzuri wa somo hili ambapo washiriki wamekuwa na maswali na michango mbalimbali. Karibu usikilize hapo chini ili ujifunze na kuchukua hatua sahihi.
View: https://youtu.be/XJ_0z7mNFGA
MJADALA WA SOMO.
Karibu kwenye mjadala wa somo hili, shiriki kwa kutuma majibu ya maswali haya;
1. Nini maana ya uhuru wa kifedha? Kwako uhuru wa kifedha ni kuwa na uwekezaji wa kiasi gani?
2. Ili ufikie uhuru wa kifedha ndani ya hii miaka 10 ya NGUVU YA BUKU, unapaswa kuwekeza kiasi gani kila mwezi?
3. Kama kiasi unachowekeza sasa hakijafikia unachopaswa kuwekeza ili ufikie uhuru wa kifedha ndani ya miaka 10, ni hatua zipi unachukua ili kufikia kiasi hicho? Na lini utakuwa umefikia?
4. Baada ya kufikia uhuru wa kifedha, nini kitakachokufanya uendelee kuwekeza?
5. Karibu kwa maswali, maoni, mapendekezo na shuhuda kuhusu somo hili na programu nzima ya NGUVU YA BUKU na UHURU WA KIFEDHA.
Tuma majibu ya maswali hayo kama uthibitisho wa kusoma, kuelewa na kutekeleza somo hili la uwekezaji.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com
www.amkamtanzania.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.