Je NI LINI SHERIA YA KUBADILISHA MAJINA YA MAKAMPUNI YA KIBIASHARA ITAKOMESHWA

Je NI LINI SHERIA YA KUBADILISHA MAJINA YA MAKAMPUNI YA KIBIASHARA ITAKOMESHWA

bily

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2012
Posts
8,029
Reaction score
5,796
Habari wanajamvi,

Ningependa kujua ni lini ile sheria ya kua kila kampuni ya kibiashara ambayo inataka kuwekeza katika sekta yoyote ni lazima ipewe miaka kadhaa ili baadae ndio ianze kulipa kodi hasa kampuni hizi za kigeni? je hatuoni kwamba tunapoteza hela nyingi sana ambazo zingesaidia kununua vyandarua kuliko kutegemea Wamarekani waje watusaidie? kuongeza madawa mahospitalini na kuwatibu wazee na wanawake wajawazito bure?

Yafuatayo ni baadhi tu ya makampuni ambayo yamewai kubadilisha majina;ZAIN-AIRTEL, KILIMANJARO KEMPISK,MOVIN PICKna mengineyo .




"ili nchi yoyote iendelee ni lazima kuwepo na uongozi bora, ardhi, watu na siasa safi" mwl Julius Nyerere
 
Kwa Muda mrefu nimekuwa nikiona watu mbalimbali wakishindwa kutofautisha kampuni kubadili jina (trade mark) na swala zoma la ulipaji wa kodi TRA. Kwa ufupi makampuni hayo iwe hoteli ama zinginezo hutambulika pale TRA kwa kutumia TIN number (Taxpayers Identification Numbers), na kubadilika kwa jina la kampuni haliisababishi/ kuizuia serikali kupitia TRA kukusanya kodi. TRA kwa mtazamo wangu ina wataalamu wazuri tu wa kodi na kwa kifupi exemption kwa miaka ya hivi karibuni zimekuwa hazipatikani isipokuwa kwa wawekezaji ambao wanawekeza kama strategic investors kupitia EPZ (Export Processing Zones). Finance Act ya mwaka 2012 iliongeza kifungu cha sheria ya kutoa msamaha huu wa kodi kwa investors ambao wanawekeza kwenye EPZ ili makampuni mengi yaje kuwekeza nchini na pia kutengeneza ajira kwa wingi kwa watanzania. Ajira hizi kwa wazawa huchangia pato serikalini kupitia kodi za PAYE (Pay As You Earn) na SDL (Skills Development Levy) kwenye mishahara yao.

Pia ikumbukwe kampuni inapouza bidhaa zake nje kwa wingi, inapata fedha za mauzo (sales revenue) na pia serikali inapata kodi "corporate income tax" ya asilimia 30% kwa faida itakayopatikana na mauzo hayo baada ya kutoa gharama zote za uendeshaji wa kampuni hiyo. Muda umefika sasa kwa idara ya elimu ya TRA kutoa elimu ya kodi kwa watanzania ili waelimike kuhusiana na hili. Mara nyingi nimekuwa najisikia vibaya hasa ninapoona kuna upotoshwaji mkubwa sana unaosababishwa na watanzania wenzangu kutokuelewa maswala haya ya kodi. Kwa ufupi, hakuna uhusiano baina ya ukwepaji wa kodi na kampuni kubadilisha jina lake la Kibiashara na hayo ma-hoteli uliyoyataja yanalipa kodi kwa kutumia TIN numbers zao na majina halisi yaliyofanyiwa usajili wa kufanya biashara hapa nchini.
 
Back
Top Bottom