Je ni lini Tanzania itaweza kurusha satellite angani?

Siku rais ALIYESUKUMIZWA akiondoka madarakani
 
mtoa mada umefikilia vizuri ila mambo haya yanahitaji support kubwa, kwa hapa kwetu politics imetawala sana.
 
Je,hizo satellite walirusha wenyewe au waliwalipa space agencies wawarushie?.Maana najua project za kurusha satelite wenyewe ni gharama kweli kweli.Maana kuunda yale ma space rockets ya kubebea satellite sio mchezo.Ni mapesa mengi sana yanahitajika.
 
Ni kuamua tu,Just kuwalipa space agencies kama Space X waturushie.Pesa tu ndo inaongea hapo
 
Profesa wa Tanzania ni wa kisiasa zaidi, wangekua wasomi hasa wangehama nchi
 
Je,hizo satellite walirusha wenyewe au waliwalipa space agencies wawarushie?.Maana najua project za kurusha satelite wenyewe ni gharama kweli kweli.Maana kuunda yale ma space rockets ya kubebea satellite sio mchezo.Ni mapesa mengi sana yanahitajika.
Ni kweli kiongozi kurusha satellite ni gharama kubwa sana, hizo nchi asilimia kubwa wameshirikiana na mamalaka za anga za mataifa kama Japan, Russia, Marekani n.k. Basi tujaribu hata kama Ghana kwa bajeti ya Dola 50,000 ni msaada mkubwa kwa taifa letu.
 
Hii ni picha tosha kuwa wenzetu wana bajeti za kufanya tafiti na pia wana sponsor wananchi wao kwenda kusoma maswala ya anga kwa ajili ya kuliletea tija taifa lao.Nadhani huu ndio wakati wetu kuanza, tunaweza anza hata na mitaala kwenye vyuo vyetu kozi hizi za maswala ya anga.

Hizi ni mamlaka za maswala ya anga kwa nchi za Africa.
  • Africa kusini -The South African National Space Agency (SANSA)
  • Misri -National Authority for Remote Sensing and Space Science
  • Nigeria- National Space Research and Development Agency
  • Algeria -Algerian Space Agency
  • Tunisia -National Remote Sensing Center of Tunisia
  • Morroco- Royal Centre for Remote Sensing
 
Ni kweli mkuu,hasa communication satellite itaturahisishia sana.
 
Tutatumia hizohizo za wenzetu, kwanza huko juu yatakuwa mengi mno yatazuia mvua na yatasababisha joto na mawingu kukimbia. Hao waliorusha yanatosha. Siye hamna haja.
Mmeshindwa kuweka taa za barabarani kuongoza magari mtaweza kurusha satellite???
Kutwa matrafik wana zungusha mikono njiapanda.
 
Tanzania inaruhusu watu binafsi kumiliki space Agencies kwa research na Technology development
 
Unazungumzia Tanzania hiii hiiii au
 
Hata ikirushwa mtasema mbovu nati zimelegea..
wabongo mna jema...., mtauliza hata hizo pesa alikozitoa Mkuu mpaka akapata za kurusha satellite
 
Unazungumzia Tanzania hiii hiiii au
Ni Tanzania hii hii mkuu, hao walioendelea kuna mahali walianzia na sisi ndiyo tumeshaanza hatua ya kwanza, badala ya kuwa negative, hebu tuunganishe mawazo, nguvu na rasilimali kwa pamoja na tusema sasa yatosha! hatutaki kununua, kuuza na kutumia (kwa mfano) Smart phone toka ughaibuni, tunataka kutengeneza zetu wenyewe na sisi ndiyo tuwauzie majirani zetu. ili kuwezesha hili kumeanzishwa klabu maalum kwa ajiri ya kuwaunganisha watanzania wa kada mbalilmbali ili waweze kushiriki kwa kutoa maoni ya kuboresha au hata kufanya kile ambachi wanadhani kitaipeleka tanzania kwenye level ya juu kabisa ya teknolojia. kwa habari zaidi tembelea hapa
ESTA -TANZANITE CITY OF TECHNOLOGY & INNOVATION: MBEYA: FRIENDS CLUB OF THE TANZANITE CITY
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…