Fafanua vizuri ni Harrier ya mwaka gani, ukubwa wa engine yake, ili tuweze kukusadia.
Nyongeza:
Ulaji mwingi wa mafuta kwenye Magari unategemea na mambo mengi sana kwenye gari.
Kifupi kwenye Harrier(haswa za 2005-2008 n.k), kinachofanya gari hii kutumia mafuta zaidi ya magari mengine yenye ukubwa sawa wa Engine CC ni udogo wa Gear Box yake, yaani ina gear 4 tu wakati huo huo ina speed 180km/Hr. Kwaiyo ECU yake inahold gear moja kwa sekunde nyingi sana yaani kuna muda ili uweze kugain speed. Pia unaweza ukawa upo kwenye speed ya 50 - 70 Km/Hr halafu upo kwenye Gear namba 3 yaani mpaka ufikie hiyo gear namba 4 wakati huo huo gari inaspeed ya 180 Km/Hr ulaji wake wa mafuta unakua mkubwa sana wakati huo.