Je ni maneno ya kweli au ni propaganda?

aleesha

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
798
Reaction score
1,178
Kuna baadhi ya wauzaji au madalali wa Magari wanasema Gari ambayo ni 4Wd sio nzuri kwasababu zifuatazo.

1. Zinakunywa sana Mafuta
2.Utengenezaji wake unakuwa mgumu.

Hapo nazungumzia kwa upande wa Zanzibar,tena kwa baadhi ya Yadi ambazo ni maarufu.

Kwa mfano Dalali anaweza kukuambia kwamba Gari aina fulani ni nzuri lakini shida yake ina 4Wd labda uitoe.

Mimi sio mtaalamu wa Magari wala sio mpenzi wa kuendesha Magari sana,lakini inapobidi na hapa sio kwamba naihitaji hapana! nataka tu nipate elimu.

Kwanza sielewi maana ya 4Wd kwamba kazi yake ni nini? kuna faida gani kuwa na Gari ya namna hiyo,lakini tofauti kati ya Gari ambayo sio 4Wd ni ipi?

nimejiuliza pia kwamba,je ikiwa mafundi wanaweza kutoa huo mfumo wa 4Wd si wataiharibu Gari?😳

Shukran
 
Wajuzi wanakuja kukupa miongozo.

TULIA HAPOHAPO.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
 
Inategemeana kuna 4wheel ya moja kwa moja ambayo hauwezi kuibadili (yani inakuwa ni 4wheel automatic mda wote ipo automatic).

Na kuna 4wheel ambayo ni Manual Hii Ipo Sana Kwenye Suzuki Escudo Zile Old Model Kabisa Zina Gia Kabisa Ya 4wheel na Hasa Ukiikuta Ile Yenye Engine ya 4 cylinder Yenye Cc 1780 Mafuta Haitumii Mengi Tofauti na Ile V6.

Na Kuna 4wheel Ambayo Ni Automatic any Time hii Ipo Sana Kwenye Noah Sr50 yenye Engine Ya 3s-fe yani mda wote Gari inakuwa ni automatic huna option ya kujichagulia iwe 4wheel au 2wheel Hii Wengi Hulalamika Hutumia Mafuta Mengi Japo Mimi Napingana Nao Maana Nimeitumia haili mafuta Mengi kiivo ni kawaida tu.

Ni Hayo Tu[emoji120][emoji593][emoji593][emoji593][emoji593][emoji593][emoji593][emoji593][emoji593][emoji593][emoji593]
 
Hakuna gari inayokunywa supu.. hiyo gari ni 4WD au AWD

Gari ya aina gani ambayo unataka kununua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…