Je, ni Mbao gani nzuri kwa ajili ya kuchongesha kitanda?

Je, ni Mbao gani nzuri kwa ajili ya kuchongesha kitanda?

commm

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2019
Posts
1,709
Reaction score
1,963
Wakuu kwa wale wataalamu wa furniture, hivi ni mbao gani nzuri kwa ajili ya kuchongesha kitanda.

Maana kuna kitanda fulani nilinunua, sasa kile kitanda kishaanza kuliwa na wadudu.

Yaani kishaanza kumwaga unga unga fulani hivi.

Sasa, kwa mwenye experience na hivi vitu labda anaweza kushare hapa jukwaani.

Ni mbao gani inafaa kuchongesha kitanda size 4 kwa 6 au 5 kwa 6.

Pia nikijua na gharama itakuwa vizuri zaidi.
 
Kwa hapa Tanzania mbao daraja la kwanza ni mninga, mvule, Mkongo etc lakini bei ya mbao umesimama si chini ya elfu 30 au zaidi kwa mbao moja. Hivyo watu sasa wanatumia mtondoro, msederela n.k
 
Tumia mti wa Mwarobaini ila uwe umekomaa vizuri hutajutia!
Hagusi mdudu wa aina yoyote hapo.
Mimi nilitebgenezewa na bro wangu tangu mwaka 2008 mpaka leo kama kipya yaani
 
Back
Top Bottom