Je, ni mtego au sumu gani ya kuwaua au kuwafukuza wadudu wasisogelee shamba la tikiti?

Je, ni mtego au sumu gani ya kuwaua au kuwafukuza wadudu wasisogelee shamba la tikiti?

Stretcher

Member
Joined
Oct 24, 2020
Posts
34
Reaction score
24
Habarini,

Nimelima tikiti zinatambaa sasa, nilishawahi kuli a mara kadhaa na nikavuna.

Changamoto iliyopo inayonifanya niombe ushauri kwenu ni kwamba tikiti zinapoanza kukomaa Kuna viumbe aina mbalimbali wanaofanana na mbea hung'ata tikiti, hungofoa tikiti na kulitoa penbeni na shamba na kulila, kama tikiti ni kubwa sana hulila humohumo ila mara nyingi mno hubeba tikiti nje ya shamba na kulila.

Wanyama hawa baadhi yao wenye aina moja hujisaidia sehemu moja haijalishi amebannwa akiwa umbali gani lazima aje anapo yea ndipo anye halafu ni usiku.

Je, ni mtego au sumu gani ya kuwaua au kuwafukuza kabisa wasisogelee shamba la tikiti? Kumbuka nikiwatega na sumu ya panya hawali, wananusa kama mbwa na kuacha tikiti ulilowategea.

Nawasilisha.
 
Niliwahi kupata hiyo kadhia
Kijana wa shamba anasema alotafuta mahali hujificha akakuta kichuguu, akachomea tairi hapo kwenye mashimo ya kichuguu akamwaga na petrol na oli chafu, aliua majoka na hao wanyama pia ndio akakomesha kwa style hiyo
 
Back
Top Bottom