Je, ni namna gani sahihi ya kumeza dawa za vindonge 2x3?

Je, ni namna gani sahihi ya kumeza dawa za vindonge 2x3?

Joined
Oct 6, 2024
Posts
147
Reaction score
303
Wazee wenzangu na wajukuu zangu salaam.

Naomba tujuzane namna sahihi ya kumeza dawa maarufu kama kutwa mara tatu.

1. Je, nigawe masaa 24/3=8 ambapo ninywe dawa kila baada ya masaa nane, yaani kama dawa nilianza kumeza saa 12 asubuhi, nije kumeza saa nane mchana, na kisha nije kumeza saa nne usiku?

2. Au kama nimeanza kumeza dawa saa 12 asubuhi, nimeze tena saa sita mchana, kisha saa 12 jioni?

Kati ya njia hizo mbili, ipi ni sahihi kwa matumizi sahihi na yenye tija kwa afya?
 
Kiufupi kila dawa iko na taratibu ya kutumiwa, nazungumzia hizihizi za 2×3.
Iko dawa haitakiwi meza night.
Hivyo ukiwa kwa nane lazima ifikie kwa night only. Hivyo iko dawa yenyewe ni mchana pekee. Hii utakula kwa kugawa masaa manne itategemea na ukali wa dawa na maelezo ya daktari,. Japo aina hii ya dawa mingi huwa ni ×2.
Pia iko dawa kabla ya kula haitakiwi ule, pia iko dawa ule baada ya kula launch.
 
Habari,
Kwa hali ya kawaida inapaswa ugawanye 24/3 =8, hivyo unywe kila baada ya masaa nane tangu ulipokunywa mara ya mwisho.

Njia hii (2x3) ya kuandika 'frequency' haishauriwi sana kwenye tasnia ya afya, lakini inasaidia mgonjwa kuelewa kirahisi (imezoeleka hivyo)

Inatakiwa kuandikwa : vidonge 2 kila baada ya masaa 8
 
Back
Top Bottom