Kiswahili Sanifu ni 'ndio', matamshi na maandishi ya 'ndiyo' yanatumiwa sana na wasemaji wa Kiswahili ambao wameathiriwa sana na lugha ya Kiarabu mf. Unguja.
Kuhusu usahihi, namna zote ni sahihi.
kiingereza kina neno center na centre....yote hutamkwa sawa na humaanisha jambo moja.hii inaletwa na utofauti katika utamshi.wakati wamarekani hutafuna neno la mwisho muingereza na wale wazungumzao British Eng husema neno lote.....mfano neno better husemwa kama berrer.iwapo mtu ambae hajui lugha ya kiingereza akiambiwa aandike better iliyotamkwa na mmarekani atagota kwenye bera...wakati aakiongea Reynold gerrad ataandika beta.....
tukija kwenye ndio na ndiyo.si mtaalamu wa lugha lakini nafahamu kuwa kiswahili kina lahaja mbalimbali.watu wa visiwani hasa unguja ambao lahaja yao ndio ilionekana kukubalika na wengi wakati wa harakati za kuifanya lugha iwe lugha inatumia neno ndiyo na sio ndio.
waandishi wengi walitoka pwani ama kufunzwa na walimu wa pwazni.hii ilitoa nafAsi kwa neno ndiyo kutumika zaidi kwenye uandishi.makabila mengi hayana yo ama ye hivyo kwenye uongezi bado ilibaki ndio.
kutokana na wingi wa watumiaji maneno haya yote huonekana sahihi....
Yote ni sahihi kutegemieana na muktadha. Kwa mfano:
Mtu: Umemwona kijana aliyevaa nguo nyeusi maeneo haya?
Mtu 1: Ndio, nimemwona.
Hapa 'ndio' imetumika kama jibu, na sijui kama unaweza kutumia ndiyo kama jibu. Na "ndiyo" inaweza kutumika katika mazingira kama: Kushindwa kutofautisha kati ya "ndio na ndiyo" ndiyo sababu iliyonifanya kuleta mjadala huu hapa. Na ndio maana watu wanachangia. Mimi naweza kuzitofautisha kama hivyo mkuu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.