Kwa sasa tumefika pagumu wote tunajiuliza nini tatizo kwenye uchaguzi wetu. wapo wanaodai kuwa uchaguzi ulifanyika kwa haki na wapinzani kushinda miaka ya 2010 hadi 2015 kupitia sheria hizi hizi za uchaguzi tulizo nazo je kwa sasa kulikoni?
Je, mfumo umebadilika au kipindi hicho Rais aliyekuwepo madarakani JK alikuwa na utashi wa kisiasa kutekeleza demokrasia na kupelekea kuwepo uchaguzi huru, haki na usio na upendeleo. Sasa hakuna utashi huo.
Je, kipi kilicho muhimu ni Utashi au mabadiliko ya katiba na mifumo, hapa wapinzani watafakari na kupigania kilicho sahihi na kitakacholeta matarajio chanya. Hapa 4R zilionyesha dalili njema za utashi wa kisiasa lakini zimefifisha matumaini.
Je, ndani ya Serikali kuna wanaopinga dhana hii kimya kimya. je wananchi wako upande gani wanasemaje, je tukubaliane wananchi wanakiona kinachofanyika kwenye uchaguzi.
Je, ushahidi wa askari Kiondo kuwa na sisi tumo akiwa na mtutu wa bunduki. Twende na kauli hiyo. Kama Taifa tutafakari kwa kina na tupate suluhisho.