Je ni sahihi deni la mzazi kuhamishiwa mtoto

Je ni sahihi deni la mzazi kuhamishiwa mtoto

richad

Member
Joined
Jan 13, 2019
Posts
14
Reaction score
3
Habari za saizi wana jamiiforums natumaini mu wazima wa afya, ngoja niende moja kwa moja kwenye mada husika

Eti kwa mfano mzazi wako alikopa fedha kwenye taasisi zinazokopesha fedha, akashindwa kulipa deni hilo akaondoka nyumbani bila taarifa yeyote sasa wale wanakikundi wenzake wakaanza kukudai wewe mtoto wake pesa za marejesho za mkopo wa mzazi wako ni haki kweli kwa hilo, ilihali kuna vitu ambavyo aliweka dhamana ambavyo ni vitu vya ndani lakini wao wanakuja nakukuambia ya kwamba aliweka nyumba yake kama dhamana ili hali unafahamu ya kwamba aliweka vitu vya ndani. Sasa wanaenda mbali zaidi nakutaka fedha ambazo wapangaji wa nyumbani kwenu wanazolipa kodi eti ziwe zinaenda kwenye marejesho moja kwa moja,

Naombeni ushauri katika hilo make bado sijachukua hatua yoyote!

Je niende kuwashitaki au ni haki kisheria wao kufanya ivyo kuingilia mambo ya kifamilia hasa kwenye nyumba ilihali katika mkopo dhamana akuweka nyumba, naombeni ushauri wenu wana JF
 
Habari za saizi wana jamiiforum natumaini mu wazima wa afya ,ngoja niende moja kwa moja kwenye mada husika

Eti kwa mfano mzazi wako alikopa fedha kwenye taasisi zinazokopesha fedha,akashindwa kulipa deni hilo akaondoka nyumbani bila taarifa yeyote sasa wale wanakikundi wenzake wakaanza kukudai wewe mtoto wake pesa zamarejesho za mkopo wa mzazi wako ni haki kweli kwa hilo...
Hawana uhalali kisheria wakufanya wanachokifanya. Ikiwa makubaliano yalikuwa nikuweka dhamana vitu vya ndani swala la nyumba na wewe kudaiwa pesa yamarejesho halikubaliki kabisa kisheria.

Kama wanahitaji kurejesha pesa yao basi warejee kwenye terms za mkata. Ambapo kilicho tumika kama dhamana nivyombo vya ndani na si nyumba.

Wazuie kufanya wanayoyafanya haraka iwezekanavyo.
 
Nenda kwenye ofisi ya wakili, lipa consultation fee, utasaidiwa.
 
Wana uthibitisho wa hati/leseni ya nyumba?

Lakini kwa busara tu kama mzazi alikopa kweli na nyumba ni ya mzazi na kuna wapangaji, kubaliana nao ulipe kadiri ya kodi zinavyopatikana maana sioni mantiki wala utu wa kutaka kuweka msuli wakati hilo deni ni halali.

Wewe unakubali wachukue vitu vya ndani? Fedheha hiyo mkuu
 
Hawana uhalali kisheria wakufanya wanachokifanya. Ikiwa makubaliano yalikuwa nikuweka dhamana vitu vya ndani swala la nyumba na wewe kudaiwa pesa yamarejesho halikubaliki kabisa kisheria.

Kama wanahitaji kurejesha pesa yao basi warejee kwenye terms za mkata. Ambapo kilicho tumika kama dhamana nivyombo vya ndani na si nyumba.

Wazuie kufanya wanayoyafanya haraka iwezekanavyo.
Sawa mkuu nashukuru sana
 
Wana uthibitisho wa hati/leseni ya nyumba?

Lakini kwa busara tu kama mzazi alikopa kweli na nyumba ni ya mzazi na kuna wapangaji, kubaliana nao ulipe kadiri ya kodi zinavyopatikana maana sioni mantiki wala utu wa kutaka kuweka msuli wakati hilo deni ni halali.

Wewe unakubali wachukue vitu vya ndani? Fedheha hiyo mkuu
Uthibitisho wa hati hawana kaka,hati ya nyumba ninayo Mimi lakin nashangaa wanaanza kuniambia ya kwamba aliweka nyumba ilihali ye mwenyewe mzazi alisema ajaweka na hati akanikabizigi mapema sana mkuu
 
Habari za saizi wana jamiiforum natumaini mu wazima wa afya, ngoja niende moja kwa moja kwenye mada husika

Eti kwa mfano mzazi wako alikopa fedha kwenye taasisi zinazokopesha fedha,akashindwa kulipa deni hilo akaondoka nyumbani bila taarifa yeyote sasa wale wanakikundi wenzake wakaanza kukudai wewe mtoto wake pesa zamarejesho za mkopo wa mzazi wako ni haki kweli kwa hilo, ilihali kuna vitu ambavyo aliweka dhamana ambavyo ni vitu vya ndani lakini wao wanakuja nakukuambia ya kwamba aliweka nyumba yake kama dhamana ili hali unafahamu ya kwamba aliweka vitu vya ndani. Sasa wanaenda mbali zaidi nakutaka fedha ambazo wapangaji wa nyumbani kwenu wanazolipa kodi eti ziwe zinaenda kwenye marejesho moja kwa moja,

Naombeni ushauri katika hilo make bado sijachukua hatua yoyote!

Je niende kuwashitaki au ni haki kisheria wao kufanya ivyo kuingilia mambo ya kifamilia hasa kwenye nyumba ilihali katika mkopo dhamana akuweka nyumba,naombeni ushauri wenu wana jf
Dawa ya deni ni kulipa, kubali tu hela ya pango iende huko alikokopa mzazi wako. Hapo mtaishi kwa amani na mzazi atarudi akiwa huru baada ya deni kuisha kabisa.
Lipeni deni hilo

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sawa mkuu ngoja nifikirie pia kwa hilo
 
Dawa ya deni ni kulipa, kubali tu hela ya pango iende huko alikokopa mzazi wako. Hapo mtaishi kwa amani na mzazi atarudi akiwa huru baada ya deni kuisha kabisa.
Lipeni deni hilo

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Shida pia mkuu wanaotaka kufanya hivyo sio taasisi husika bali ni wanakikundi wenzie wachache wengine wamekaa kimya tu mkuu,bora hata ingekuwa taasisi yenyewe ndo inataka kufanya hivyo lakini sasa sio wao? Je nitawaamini vipi kiongozi kama pesa hiyo ikitoka itaenda moja kwa moja kwenye marejesho,na ilihali pia hata wakichangia deni hilo likaisha bado mzazi akirudi atalazimika kuwalipa wahusika wenzake pesa ambayo walimchangia kipindi ambacho ametoka, sasa hapo kipi bora nikubali au nikatae ili tuje kuwalipa baadae mkuu! Ushauri wako kwa hilo tafadhali
 
Back
Top Bottom