Je, ni sahihi Kituo cha Polisi na Polisi kuwa Chombo cha Usuluhishi wa migogoro ya kijamii?

Je, ni sahihi Kituo cha Polisi na Polisi kuwa Chombo cha Usuluhishi wa migogoro ya kijamii?

Uwesutanzania

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2019
Posts
1,380
Reaction score
1,686
Kum-radhi kama bandiko langu litakuwa na maana/maudhui ya tofauti na kuhitaji kufahamishwa na kuelimishwa.

Ni mimi wako UWESUTANZANIA.

Katika jamii nyingi na maeneo tofauti tofauti hapa nchini kwetu kumekuwa na desturi ya watu kukimbilia polisi na polisi kupokea na kusikiliza kesi hata ambazo sio za makosa ya JINAI.

Utakuta mtu anamigogoro ya kifamilia na familia yake basi mtu huyo anaenda polisi na polisi wanaipokea kesi hiyo nakuisuruhisha tena utakuta mgogoro wala hauna jinai ndani yake.

Bodaboda sijui anadaiwa hesabu na muajiri wake kesi polisi, Shamba na shamba kiwanja na kiwanja kesi polisi,
Familia sijui mtoto atekelezi nini na nini kesi polisi.

Na polisi wenyewe wala hawana pingamizi katika haya, Siku izi wanafika mbali mpaka kesi za mwanafunzi na mimba wanamaliza wao,.

Yaani mpaka ukiona jambo linaenda mahakamani basi ujue wenda mmoja wa wanakesi naomba mwenyewe ipelekwe mahakamani.

Je, hii sio kuwashusha hadhi mapolisi na kituo cha polisi?

Au hii nikuwapandisha hadhi na kufanya wenye daraja la juu kwa wao kufanya hivi?

Nahitaji tu kujua asante.
 

Attachments

Back
Top Bottom