star health talks
Member
- Apr 28, 2017
- 30
- 73
Uji wa lishe ni nini; ni uji unaotengenezwa kwa kutumia nafaka mbali mbali zilizochanganywa na virutubisho vingine mfano protini, mafuta n.k
Je, ni sahihi kumpa mtoto; ndio, mtoto kuanzia umri wa sita na kuendelea anaweza kupewa
Ni makosa gani tunayoyafanya mara kwa mara, unga wa lishe wa kawaida mtaani utakuta kuna mchanganyiko wa mahindi, mtama, mchele, ngano, soya, mbegu za maboga na karanga, wengine wanaenda mbali na kuweka na dagaa.
Kama unakumbuka biologia kidogo utakumbuka mahindi, mtama, mchele na ngano vyote ni wanga, kazi yake ni moja, hivyo haina haja ya kuvichanganya kwa pamoja sabau haina faida yoyote kitaalam
Kwanini wataalam wa afya hususani madaktari bingwa wa watoto hawapendekezi mchanganyiko wa aina hii
Nini kifanyike?

- Moja, mchanganyo wa aina nyingi ya nafaka na vitu mbali mbali inapoteza ladha ya uji mwenyewe, emu jitafakari we ndo unakunywa huo uji
- Mtoto anakuwa anakunywa au kula aina moja tu ya chakula yaani wanga, huku akikosa virutubisho muhimu kama protein n.k, kumbuka mtoto mdogo anahitaji protein kwa kiasi kikubwa kuliko wanga
- Unga wa lishe uliotengenezwa kwa ain hii hasa kama ulichanganywa na karanga kabla ya kusagwa unawahi kuoza, maana karanga zinawahi kuoza na kutengenea sumu inayoitwa “afflatoxin” kwa kitaalam, hii huweza kusababisha ini kufeli huko mbeleni
- Nafaka mbali mbali zinazokuwa zimechanganywa zinapikika na kuiva katika joto tofauti, wenzagu mliosoma kemia mtakumbuka kitu kinaitwa boiling point, yes different cereals have different boiling point, maana yake ni kuwa baadhi ya nafaka zitapiikia sana na kupoteza ubora na nyingine hazitaiva sawa sawa,
Nini kifanyike?
- Moja, tengeneza unga wa uji kwa kutumia nafaka aina moja, ambayo unaweza kuibadilisha kila unaposaga unga ili kubadilisha ladha, mfano mwezi uji andaa unga wa mahindi pekee, mwezi mwingine ngano, muhogo n,k, kisha ukisha pika uji ongeza vitu vya protein kwa kukorogea kwenye uji mfano siagi, peanut butter, bleuband
- Mtoto asinywe uji peke yake kila siku, kulingana na umri wa mtoto, anaweza kunyonya maziwa ya mama, kula vyakula vya makundi tofauti tofauti kulingana na umri aliokuwa nao