Starlet iko vizuri sana kwa misele ya town.
Number siyo issue chukuwa fundi aikaguwe injini kama haina tatizo chukuwa gari hiyo.
Mimi siyo muosha kinywa nayaelewa magari, gari yangu ya kwanza 504 guruwe nimeanza kumiliki mwaka 2000.
Mimi nilikuwa na Toyota Surf nilimuuzia mtu ina namba A huku roho inaniuma maana nilibadirisha injini nilitowa 2L na nikaweka injini ya 1kz zile za Land cruiser, kwahiyo niliyemuuzia ile gari leo ukimuuliza swali kama hili lako atakucheka.
Nimeona nikupanuwe ufahamu kidogo uelewe elimu ya magari, unaweza kuuziwa gari namba C na mchaga ukakuta ni bora hata hilo namba A maana mchaga kila msiba moshi ataenda na hiyo gari kila dharura yuko moshi na gari, kwa kifupi mimi siwezi kununuwa gari kwa mchaga.