Je, ni sahihi kwa mwanaume kuwa na mke mmoja? Kwanini wanaume wengi hawariziki na mwanamke mmoja?

Kisa nini sasa mpaka ban imeusika
Hahahaaa hukuepo ile Siku??? lol Hawa jamaa seems wamevurugwa sio kidogo... na hapa hawachelewi kutupin ndugu mjumbe.

Kuna vagi lilitokea juzikati ni muendelezo wa yalee mabishano ya ile siku nadhani hata wee ulichangia kidogo. Sasa keshoyake ndio kulikuchaaa pale hadi Watu wakakimbilia kuomba msaaada kwahawa jamaa watoa pin!
 
Kuwa na mwanamke mmoja ni unyonge na udhaifu. Ila nakukumbusha tu "Usishindane na Ulikotoka"
 
Bible imeandikwa mmeo mmoja na mke mmoja lkn hawatimiziani matakwa🥱
 
Nikurekebishe sio kweli kuwa idadi ya wanawake nikubwa Sana kuliko wanaume hizo ni story za vijiweni. Duniani idadi ya wanaume nikubwa kuliko wanawake Tena tumewapita kwa uchache wanawake wakiwa 3.99B wakati wanaume tukiwa 4B
 
Kuwa na mke mmoja ni kosa kwa Mungu, wengine atawaoa nani? Kulingana na uumbaji wa Mungu, hakika mwanaume hatosheki na mke mmoja. Waulize Waislamu.
 
Jirani yangu mmoja ana mke wa ndoa na watoto lakini kazaa na housegirl wake.Mtoto anamficha eti isije julikana kanisani akatengwa na akakosa ule mkate.
Kati ya huyu na mvaa kobaz kaamua kuhalalisha je ni nani mnafiki mbele za mungu
 
Mungu ndiye mwanzilishi wa ndoa ya mke MMOJA.

Binadamu ndiye mwanzilishi wa ndoa ya wake WENGI.

Wewe utamfuata yupi?
 
Mnahangaika sana, oa huyo mke mmoja ukipata tamaaa kajiridhishe urudi kwa mkeo ila tumia
Kinga na jitayarishwe kulogwa na michepuko. Sikia mwanangu kuna maisha zaidi ya mmbunye. Mke mmoja mwenyewe kumridhisha haja zake zote kipengele ndo uende kuoa wengine. Ukiangalia ndoa za wake wengi asilimia 50 wanaumwa . Huwezi ridhisha wanawake wawili kifedha au kimwili . Ni Kujidanganya tu.
Kama unataka wake wawili weka mkeo hapa tumwone hali yake kifedha kimwili kiroho na kiafya ndo tuamue sio unataka wake wengi wakati mmoja ata chupi mpya hana mdhooofu umpelekea magonjwa tu. Sijui umri huu wanaume mnawaza nini aiseee tafuteni ela mwanangu
 
Mungu ndiye mwanzilishi wa ndoa ya mke MMOJA.

Binadamu ndiye mwanzilishi wa ndoa ya wake WENGI.

Wewe utamfuata yupi?
Unauhakika imeandikwa Ivo na kama imeandikwa mbn mnatwambia mke mmoja hatoshi imekuaje tue tofauti na dini ya kislama mume kua na mke zaidi ya mmoja nao utaratibu wameutolea wapi🔥
 
Unauhakika imeandikwa Ivo na kama imeandikwa mbn mnatwambia mke mmoja hatoshi imekuaje tue tofauti na dini ya kislama mume kua na mke zaidi ya mmoja nao utaratibu wameutolea wapi🔥
Mungu alimpa Adamu mke MMOJA (Hawa/Eva)
 
Mungu ndiye mwanzilishi wa ndoa ya mke MMOJA.

Binadamu ndiye mwanzilishi wa ndoa ya wake WENGI.

Wewe utamfuata yupi?
kama ni hivyo Daudi,Mussa manabii wasingekuwa na wake wengi.
Najua unamsemea YESU yesu hakuwa mungu bali alikuwa Masiha yaani zaidi ya Nabii
YESU kutokuoa ilikuwa mipango ya MUNGU Isiwe tafsiri kwa wengine
 
Anaesema anaridhika na mke mmoja ni mnafiki, amini usiamini, hakika nawaambia, japo haijaandikwa "mwanaume hatosheki na mke mmoja " wazee wa zamani walijua hilo. Hizi imani uchwara za kizungu zimetuvuruga.
 
Ukiona unataka kuongeza mke mwingine ujue una muda mwingi wa kupoteza. Ukiwa busy na shughuli zako hata huyo mmoja unakosa nae muda, bado watoto, familia na marafiki. Jifunze kutoka Japan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…